
Yanga walishatwaa Ubingwa tangu Wiki iliyopita na Msimu ujao watawakilisha kwenye CAF CHAMPIONS LIGI na Azam FC, ambao wamepoteza Taji lao, wameshika Nafasi ya Pili na hivyo watacheza Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.
Kwa Msimu huu Timu mbili zitashushwa Daraja na Timu 4 kupandishwa ili kufanya idadi ya Timu za Ligi Kuu Vodacom kuwa 16 Msimu ujao badala ya 14 za sasa.
Timu 4 zilizofuzu kupanda Daraja na kucheza Ligi Kuu Vodacom Msimu ujao ni Majimaji ya Songea, Mwadui ya Shinyanga, African Sports ya Tanga na Toto Africans ya Mwanza.
Timu moja ambayo itaungana na Polisi Moro kuporomoka Daraja kutoka Ligi Kuu Vodacom ni moja kati ya Timu 5 ambazo ni Ruvu Shooting, Prisons, Stand United, Ndanda FC na Mgambo JKT.

LIGI KUU VODACOM
RATIBA
Jumamosi Mei 9


0 maoni:
Chapisha Maoni