.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumanne, 18 Novemba 2014

Tagged Under:

DALEY BLIND WA MANCHESTER UNITED AUMIA GOTI! KOCHA LUIS VAN GAAL KWENYE WASIWASI!!

By: Unknown On: Jumanne, Novemba 18, 2014
  • Share The Gag

  • KIUNGO wa Manchester United Daley Blind leo atafanyiwa uchunguzi wa kina wa Goti lake baada ya Jana kuumia akiichezea Nchi yake Netherlands ilipoifunga Latvia Bao 6-0 kwenye Mechi ya Kundi ya EURO 2016 iliyochezwa huko Amsterdam Arena Jijini Amsterdam.
    Blind, mwenye Miaka 24 na aliehamia Man United kutoka Ajax mwanzoni mwa Msimu, alilazimika kutoka nje ya Uwanja katika Dakika ya 20 ya Mechi hiyo na Latvia.
    Blind, ambae ameichezea Man United Mechi 8 Msimu huu, anakuwa Mchezaji wa pili wa Klabu hiyo kuumia wakati huu ambao Wachezaji wako kwenye Timu zao za Taifa kwa ajili ya Mechi za Kimataifa.

    Majuzi, Golikipa David de Gea aliteguka Kidole kidogo cha mkononi wakati akiwa Mazoezni na Nchi yake Spain.

    Jumamosi, Man United wapo Ugenini huko Emirates kucheza na Arsenal kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na upo wasiwasi mkubwa kama Blind na De Gea watacheza Mechi hiyo.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni