.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatano, 30 Septemba 2015

Tuzo nyingine zinazowahusu wakali wa Nigeria 2015, Diamond Platnumz nae yumo..!!

By: Unknown On: Jumatano, Septemba 30, 2015
  • Share The Gag
  • Ukitaja Tuzo kubwa zinazohusu Muziki wa Tanzania ni Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards… Nigeria nao wanazo za kwao, zinaitwa Headies Awards na good news ni kwamba tayari wakali wanaowania Tuzo hizo wamefahamika.. yani ile list ya Nominees wote niko nayo tayari.
    Tumeona kwa KTMA huwa inatoa Tuzo pia kwa baadhi ya wasanii wa nje, mfano kipengele cha ‘Wimbo Bora Afrika Mashariki‘… YES, Nigeria nao wana Category ya AFRICAN ARTISTE ambapo Nominees wa hapo ni wasanii wanaofanya poa kutoka Nchi mbalimbali za Afrika nje ya Nigeria.
    Category hiyo kwenye Headies Awards 2015 imewakutanisha wakali kama AKACassper Nyovest, na Uhuru toka South AfricaSarkodie wa Ghana pamoja na Diamond Platnumz toka Tanzania.
    List ya Nominees yote hii hapa mtu wangu.
    BEST RECORDING OF THE YEAR
    Ojuelegba – Wizkid
    Eyo – Asa
    Wish Me Well – Timi Dakolo
    Bez – There’s A Fire
    Cobhams – Do the right Thing
    PRODUCER OF THE YEAR
    Don Jazzy – Godwin (Korede Bello)
    Mastakraft – Wiser (Flavour)
    Young John – Bobo (Olamide)
    Shizzi – Fans Mi (DavidO)
    Legendury Beatz – Ojuelegba
    Cobhams – There’s A Fire (Bez)
    BEST MUSIC VIDEO
    This award goes to the video director.
    Jamb Question (Simi) – Mex
    Crazy (Seyi Shay) – Meji Alabi
    The Sound (Davido Feat. Uhuru & Dj Buckz) – Sesan
    Katapot (Reekado Banks) – UnLimited LA
    Baby Jollof (Solid Star Feat. Tiwa Savage) – Clarence Peters
    BEST R&B/POP ALBUM
    Bed of Stone – Asa
    A.Y.O. – Wizkid
    King of Queens – Yemi Alade
    Rich & Famous – Praiz
    Double Trouble – P Square
    BEST R&B SINGLE
    Heartbeat – Praiz
    Baby Daddy – Iyanya
    Say You Love Me – Leriq ft. Wizkid
    Do the Right Thing – Cobhams Ft. Bez
    Wish Me Well – Timi Dakolo
    BEST POP SINGLE
    Ojuelegba – Wizkid
    Collabo – P-Square Feat. Don Jazzy
    My Woman, My Everything – Patoranking Feat. Wande Coal
    Woju – Kiss Daniel
    Godwin – Korede Bello
    Bobo – Olamide
    BEST REGGAE/DANCEHALL SINGLE
    German Juice – Cynthia Morgan
    Sanko – Timaya
    My Body – Solid Star Feat. Timaya
    Daniella Whyne – Patoranking
    Cheques and Balance – Burna Boy
    Bad Girl Special (Remix) – Mr. 2Kay feat. Cynthia Morgan & Seyi Shay
    BEST RAP ALBUM
    Baba Hafusa – Reminisce
    Street OT – Olamide
    Chairman – M.I.
    Above Ground Level – Modenine
    BEST COLLABO
    Local Rapper – Reminisce Feat. Olamide & Phyno
    Hold on – Joe El Feat. 2Face Idibia
    Bad Girl Special (Remix) – Mr. 2Kay Feat. Cynthia Morgan & Seyi Shay
    Shoki (Remix) – Lil’Kesh Feat. Olamide & David O
    Do The right Thing – Cobhams ft. Bez
    Sisi – Praiz ft. Wizkid
    BEST RAP SINGLE
    King Kong – Vector
    Bad Belle – M.I
    Bank Alert – Ill Bliss
    Local Rapper – Reminisce Feat. Olamide, Phyno & Stomrex
    G.O.D – T.R
    BEST VOCAL PERFORMANCE (MALE)
    Praiz – If I fall
    Shaydee – High
    Timi Dakolo – Wish Me Well
    Cobhams – Do The Right Thing
    Bez – There’s A Fire
    BEST VOCAL PERFORMANCE (FEMALE)
    Waje – Coco Baby
    Aramide – Iwo Nikan
    Asa – Bed of Stone
    Simi – Tiff
    Yemi Alade – Duro Timi
    NEXT RATED
    Reekado Bankz
    Kiss Daniel
    Cynthia Morgan
    Korede Bello
    Lil’ Kesh
    HIP HOP WORLD REVELATION
    Praiz – Rich n Famous
    Yemi Alade – King of Queens
    Skales – Man of the Year
    LYRICIST ON THE ROLL
    Ill Bliss – Bank Alert (remix) Feat. Ice Prince, Eva Alordiah & Phyno
    Vector – King Kong
    Reminisce – Baba Hafusa
    G.O.D – T.R
    BEST STREET-HOP ARTISTE
    Reminisce – Skillashi
    Olamide – Bobo
    Small Doctor – Mosquito Killer
    Mastakraft feat. Olamide, CDQ and David O – Indomie
    Falz The Bad Guy Feat. Yemi Alade & Poe – Hello Bae
    BEST ‘ALTERNATIVE SONG
    Di’Ja – Awwwwww
    Bez – There’s A Fire
    Asa – Satan Be Gone
    Adekunle Gold – Sade
    Ugovinna – Rain On Me
    Simi – Tiff
    ALBUM OF THE YEAR
    Rich n Famous – Praiz
    King of Queens – Yemi Alade
    Street OT – Olamide
    Chairman – M.I.
    A.Y.O. – Wizkid
    Double Trouble – P Square
    ARTISTE OF THE YEAR
    Olamide
    Davido
    Wizkid
    Yemi Alade
    P Square
    SONG OF THE YEAR
    Ojuelegba – Wizkid
    Godwin – Korede Bello
    Kiss Daniel – Woju
    Olamide – Bobo
    AFRICAN ARTISTE
    Diamond Platnumz
    Cassper Nyovest
    Sarkodie
    Uhuru
    AKA
    HALL OF FAME
    2Face Idibia

    UEFA CHAMPIONS LEAGUE: MANCHESTER UNITED 2 vs 1 WOLFSBURG,

    By: Unknown On: Jumatano, Septemba 30, 2015
  • Share The Gag
  • 2-1 Smalling anagongewa kisigino na Juan Mata kama pasi ya kijanja na kufunga bao na kuwaacha mabeki wa Wolfsburg wakiduwaa! Smalling alifunga bao hilo kipindi cha pili dakika ya 53 na kuipa bao la pili Man United.David De Gea kama kawaida kufurahi Timu inapopata bao!Hoi!!1-11-1 man u penati ya mata dakika 341-11-1 Mata akishangilia na mpira baada ya kusawazishaYes! 1-1Ni balaa tupu! wote wanazo 31-0Wakijiuliza!!

    UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BORUSSIA MONCHENGLADBACH 1 vs 2 MANCHESTER CITY

    By: Unknown On: Jumatano, Septemba 30, 2015
  • Share The Gag


  • Sergio Aguero ndie aliyeipatia Man City bao kwa mkwaju wa penati usiku huu kwenye Uefa Champions League.

    Aleksandar Kolarov akishangilia na wenzake kwenye Ushindi baada ya kupata bao kwa mkwaju wa penati Man City katika dakika za lala salama.
    Martin Demichelis kwenye patashika kupata bao mbele ya Julian Korb lakini  Nicolas Otamendi alikuwepo kwenye kasi kuumalizia

    Korb akishuhudia kipute kikiziona nyavu
    Otamendi ndie aliyeisawazishia bao Man City na kufanya 1-1

    Manchester City walifungiwa bao na Nicolás Otamendi aliisawazishia bao dakika ya 65 na dakika za lala salama dakika ya 90 Sergio Agüero aliifungia bao la Ushindi Man City kwa mkwaju wa penati na kufanya 2-1. Huku bao la Borussia Monchengladbach likifungwa na Lars Stindl dakika ya 54www.bukobasports.comBorussia Mönchengladbach v Man City 

    UEFA CHAMPIONS LEAGUE: MALMO FF 0 vs 2 REAL MADRID, CRISTIANO RONALDO AFUNGA BAO LA 500!

    By: Unknown On: Jumatano, Septemba 30, 2015
  • Share The Gag

  •  Cristiano Ronaldo akishangilia bao lake baada ya kuifunga timu ya  Malmo kwenye Uwanja wa  Swedbank Stadium na huku likiwa bao lake la 500 kisoka, Dakika ya 90 pia aliipatia bao la pili Real Madrid

    1-0 Ronaldo akishangilia

    Ronaldo akizungukwa na wenzake kupongezwa baada ya kuweka historia kwenye maisha yake ya kisoka leo hii kwenye mchezo wa UEFA Champions Ligi
    Cristiano Ronaldo alifunga bao dakika ya 29 na likiwa bao lake la 500 kisoka.  Dakika ya 90 Ronaldo alifunga tena bao la pili na mtanange kumalizika kwa bao hizo 2-1.

    FULL TIME VPL: SIMBA SC 1 vs 0 STAND UNITED

    By: Unknown On: Jumatano, Septemba 30, 2015
  • Share The Gag

  • Refa ni Ahmada Simba(Kagera)

    UEFA CHAMPIONS LEAGUE

    By: Unknown On: Jumatano, Septemba 30, 2015
  • Share The Gag

  • Baada ya Jana Klabu za Jiji la London, Arsenal na Chelsea, zote kubamizwa kwenye Mechi zao za pili za Makundi yao ya UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, Leo ni zamu ya Klabu mbili za Jiji la Manchester.
    Leo, Manchester United wako kwao Old Trafford kucheza Mechi yao ya pili ya Kundi B na Klabu ya Germany VfL Wolfsburg.
    Man United walifungwa Mechi yao ya kwanza huko Netherlands 2-1 na PSV Eindhoven.

    Nao Man City, ambao wako Kundi D, walifungwa Mechi yao ya kwanza wakiwa kwao Etihad 2-1 na Juventus na Leo wako huko Germany kucheza na Borussia Monchengladbach.
    Kwenye Mechi za Jana, Arsenal walipokea kipigo chao cha pili mfululizo kwenye Kundi lao baada ya kuchapwa Uwanjani kwao Emirates 3-2 na Olympiakos ya Greece.
    Nao Chelsea, baada ya kushinda Mechi yao ya kwanza ya Kundi lao, Jana huko Ureno walipigwa 2-1 na FC Porto.

    UEFA CHAMPIONS LEAGUE
    RATIBA
    Jumatano 30 Septemba 2015
    KUNDI A

    Malmö FF v Real Madrid
    Shakhtar Donetsk v Paris St Germaine
    KUNDI B
    CSKA v PSV
    Man United v VfL Wolfsburg
    KUNDI C
    19:00 FC Astana v Galatasaray
    Atletico Madrid v Benfica
    KUNDI D
    Borussia Mönchengladbach v Man City
    Juventus v Sevilla

    VPL KUENDELEA KWENYE VIWANJA SABA, SIMBA v STAND UNITED, MTIBWA SUGAR v YANGA

    By: Unknown On: Jumatano, Septemba 30, 2015
  • Share The Gag

  • Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea leo Jumatano kwa timu 14 kucheza katika viwanja saba nchini, ikiwa ni raundi ya tano ya ligi hiyo iliyoanza kutimua vumbi Septemba 12, 2015.
    Simba SC watakua wenyeji wa Stand United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Azam FC watawakaribisha Coastal Union kwenye uwanja wa Azam Complex – Chamazi jijini Dar es salaam.
    Mjini Morogoro vinara wa ligi hiyo Young Africans watakua ugenini kuwakabili wenyeji Mtibwa Sugar ambapo timu zote zikiwa na alama 12 baada ya kucheza michezo minne zikipishana kwa tofauti ya magoli, Wana Lizombe Majimaji FC watakua wenyeji wa Ndanda FC kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.

    JUMA NYOSO AFUNGIWA MIAKA MIWILI

    Kamati ya masaa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu iliyokutana leo kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza nchini imemfungia mchezji Juma Nyoso wa timu ya Mbeya City kucheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000) kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC John Bocco.
    Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo no namba 32 wa VPL kati ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, kutokana na kuwa tabia ya kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu mara kwa mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.
    Klabu ya Young Africans imepigwa faini ya shiligi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake watano kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Simba SC. Kwa mujibu wa kanunu namba 42 (11) timu ambayo wachezaji wake watapata kadi zaidi ya tabo katika mchezo mmoja itapigwa faini ya shilingi laki tano.
    Wachezaji waliopata kadi za njano wa Young Africans katika mchezo huo ni ni Salum Telela, Mbuyu Twite, Malimi Busungu, Ali Mustafa na Mbuyu Twite.
    Aidha klabu ya Yanga imepigwa faini nyingine ya shilingi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake kwenda kushangilia upande wa Simba SC mara baada ya mchezo kumalizika.
    Mchezo utatazamwa tena ili kuangalia malalamiko ya Simba SC dhidi ya mwamuzi.
    Simba pia inapigwa faini baada ya wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwashambulia waamuzi baada ya mchezo ambapo waliwarushia chupa za maji ambazo nyingine ziliwakosa waamuzi na kumpata kocha wa Yanga Hans Van Pluijm.
    Mchezo namba 26 wa VPL kati ya Coastal Union na Mwadui uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Chumba cha Coastal Union kilikuwa na harufu kali sana. Baadhi ya mashabiki wa Coastal Union waliokuwa nyuma ya goli la upande wa kaskazini walitoa lugha ya matusi kwa waamuzi na kutishia kuwapiga na pia walimrushia mawe mwamuzi msaidizi wa pili Shafii Mohamed na jiwe moja lilimpiga mgongoni na kumjeruhi kidogo mwamuzi na aliomba msaada wa jeshi la polisi kutuliza ghasia, mchezo ulisimama kwa dakika 3.

    UEFA CHAMPIONS LEAGUE: FC PORTO 2 v 1 CHELSEA

    By: Unknown On: Jumatano, Septemba 30, 2015
  • Share The Gag

  • Ushindi!Jose Mourinho alishindwa kuamini
    Kwenye Kundi G, FC Porto, ikiwa kwao Ureno Estadio do Dragao Jijini Porto, iliicharaza Timu ya Mreno mwenzao Jose Mourinho, Chelsea, Bao 2-1.
    Bao za Mechi hii zilifungwa na Andre Andre kwa FC Porto katika Dakika ya 39 na Chelsea kusawazisha Dakika ya 45 kwa Frikiki ya Willian.
    Kichwa cha Maicon katika Dakika ya 52 kiliwapa FC Porto ushindi wa Bao 2-1.
    Katika Mechi nyingine ya Kundi hili la Chelsea, Dinamo Zagreb ilitamba Ugenini baada ya kuichapa Maccabi Tel Aviv 2-0.
    2-1
    PORTO WANAONGOZA SASA 2-1WILLIAN ALIPOISAWAZISHIA CHELSEA 1-1FC Porto v Chelsea VIKOSI:

    UEFA CHAMPIONS LEAGUE: ARSENAL 2 v 3 OLYMPIAKOS, ARSENE

    By: Unknown On: Jumatano, Septemba 30, 2015
  • Share The Gag

  • Felipe Pardo aliipa Olympiakos Bao la kuongoza lakini Theo Walcott akaisawazishia Arsenal ambao walikwenda Mapumziko wakiwa nyuma 2-1 baada ya Kipa wao David Ospina kujifunga mwenyewe.
    Kipindi cha Pili, Arsenal walisawazisha Dakika ya 65 kwa Bao la Alexis Sanchez lakini Dakika 1 baadae Olympiakos walifunga Bao la 3 na la ushindi wa 3-2 kupitia Alfred Finnbogason.
    Hii ni Mechi ya pili mfululizo kwa Arsenal kuchapwa katika Kundi F baada kupigwa 2-1 na Dinamo Zagreb na sasa wana kibarua kigumu cha kufuzu na kuwa Timu ya kwanza kufanya hivyo tangu Msimu wa 2012/13 tangu Galatasaray walipofungwa Mechi mbili za kwanza na kuweza kusonga hatua ya Mrtoano ya UCL.
    Ili kufanya hivyo, Arsenal inabidi kwanza washinde Mechi zao mbili zinazokuja na zote ni dhidi ya Bayern Munich.
    Arsenal wakubali yaishe! wapigwa bao 2-1, Wafungaji bao za Olympiakos ni Felipe Pardo 33' David Ospina 40' OG na Alfred Finnbogason 66. Bao za Arsenal zilifungwa na Theo Walcott dakika ya 35 na lile la Alexis Sánchez dakika ya 65 na mtanange kumalizika kwa 3-2 Olympiakos wakiibuka kidedea Emirates!

    Arsenal v Olympiakos

    UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BARCELONA 2 v 1 BAYER LEVERKUSEN

    By: Unknown On: Jumatano, Septemba 30, 2015
  • Share The Gag


  • Barcelona v Bayer Leverkusen
    VIKOSI:
    Barcelona:
    Ter Stegen, Dani Alves, Pique, Mascherano, Mathieu, Rakitic, Busquets, Iniesta, Sandro, Suarez, Neymar.
    Akiba: Masip, Douglas, Bartra, Munir, Jordi Alba, Sergi Roberto, Gumbau.

    Bayer Leverkusen: Leno, Donati, Tah, Papadopoulos, Wendell, Kramer, Bender, Kampl, Calhanoglu, Bellarabi, Hernandez.
    Akiba: Kresic, Ramalho Silva, Kiessling, Hilbert, Mehmedi, Boenisch, Brandt.

    Refa: Martin Atkinson

    UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BARCELONA 2 v 1 BAYER LEVERKUSEN

    By: Unknown On: Jumatano, Septemba 30, 2015
  • Share The Gag

  • Barcelona v Bayer Leverkusen
    VIKOSI:
    Barcelona:
    Ter Stegen, Dani Alves, Pique, Mascherano, Mathieu, Rakitic, Busquets, Iniesta, Sandro, Suarez, Neymar.
    Akiba: Masip, Douglas, Bartra, Munir, Jordi Alba, Sergi Roberto, Gumbau.

    Bayer Leverkusen: Leno, Donati, Tah, Papadopoulos, Wendell, Kramer, Bender, Kampl, Calhanoglu, Bellarabi, Hernandez.
    Akiba: Kresic, Ramalho Silva, Kiessling, Hilbert, Mehmedi, Boenisch, Brandt.

    Refa: Martin Atkinson