Kwa mara ya 12 sasa!! Wana Gunners wakishangilia na Kombe lao!
Giroud nae yale yale!! Mikono juu 4-0
Mzee Wenger mikono juu!!Arsenal, ambao walikuwa wakitetea Taji lao walilotwaa Mwaka Jana, walikutana na Aston Villa waliokuwa wakisaka kulitwaa kwa mara ya kwanza tangu 1957.
Lakini Msimu huu, kwenye Ligi Kuu England, Arsenal iliipiga Villa nje ndani kwa jumla ya Bao 8-0 na Fainali hii haikuonyesha hata chembe kama Villa wana ubavu wa kubadili hilo baada ya kutawaliwa Mechi nzima.
4-0
Jack W. mbele ya Mashabiki
Arsene Wenger nae mbele ya mashabiki akiwashukuru kwa yoote
Ubingwa huo!
Olivier
Giroud aliifungia bao la nne Arsenal dakika za majeruhi dakika ya 90
akipata mpira kutoka kwa Alex Oxlade-Chamberlain na kuhitimisha Mchezo
huo wa Fainali ya FA Cup kwenye Uwanja wa Wembley na mtanange kumalizika
kwa bao 4-0 dhidi ya Aston Villa. Arsenal ni Ushindi wa mara ya 12
kuutwaa wakiwazidi kete moja Magwiji wa England Man United ambao
wameutwaa mara 11.
3-0 Furaha ya Kombe hii
Baadhi ya wachezaji wa Gunners wakipongezana chini
Villa akiwa hoi baada ya kujionea kichapo!
Tim nae kachanganyikiwa!
Per Mertesacker akiliona lango la wapinzani wao!
Per
Mertesacker alifunga bao la tatu na kufanya 3-0 dhidi Aston Villa
akipata pasi kutoka kwa Santi Cazorla dakika ya 62 kipindi cha pili. Theo Walcott aliifungia bao kipindi cha kwanza dakika 40 baada ya kupata pasi kutoka kwa Alexis Sánchez.
Mpaka nyavuni!
Alexis Sánchez dakika ya 50 kipindi cha pili anaifungia bao la mbali kama yadi 30 na la pili na kufanya bao kuwa 2-0 dhidi ya Aston Villa.
Theo Walcott aliifungia bao kipindi cha kwanza dakika 40 baada ya kupata pasi kutoka kwa Alexis Sánchez.
Theo akiziona nyavu za Aston Villa
Theo Walcott akishangilia bao lake
Majonzi kilio kwa Aston villa
Kipindi cha kwanza kinaendelea..
Chupuchupu!
Hector akiwekewa ngumu na mchezaji wa Aston Villa



0 maoni:
Chapisha Maoni