Raha ya Ushindi!Alexis Sanchez ndie aliyeipa ushndi Gunners leo dhidi ya Timu ya Reading
Mabingwa Watetezi wa FA CUP, Arsenal, Leo hii Uwanja wa Wembley Jijini London, wameichapa Timu ya Daraja la chini la Championship, Reading, Bao 2-1 katika Nusu Fainali ya FA CUP.
Pasi safi ya Mesut Ozil ndiyo iliyompa nafasi Alexis Sanchez kuipa Bao la kwanza Arsenal Dakika ya 30 Bao ambalo lilidumu hadi Mapumziko.

Reading walisawazisha katika Dakika ya 54 kwa Bao la McCleary alieunganisha krosi ya Pogrebnyak kutoka kushoto kwa Goli.
Hadi Dakika 90 kumalizika Gemu ilikuwa 1-1 na kuongezwa Dakika za Nyongeza 30.
Alexis Sanchez aliipa Arsenal Bao la Pili na la ushindi katika Dakika ya 106 baada ya Shuti lake kumpenya Kipa Federici.
Nusu Fainali nyingine itachezwa Kesho, pia Uwanjani Wembley, kati ya Aston Villa na Liverpool.
Alexis
Sánchez dakika ya 39 kipindi cha kwanza aliip Arsenal bao la kuongoza
kwa kufanya 1-0 dhidi ya Readinng na kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza
kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili dakika ya 54 Garath McCleary aliwasawazishia bao Reading na kufanya 1-1.

Kwenye muda wa ziada dakika 30 ili kuhitimisha dakika 120 dakika ya 105 Sánchez aliwaongezea bao la pili Arsenal na kufanya bao kuwa 2-1
Giroud akifanya yake
Kipa wa Reading akiuweka kwapani mpira uliopigwa na Giroud
Patashika
Aaron akipagawa baada ya kukosa nafasi ya wazi leo hii
Kipa wa Reading akiwa kwenye kibarua
Garath McCleary aliposawazisha bao dakika ya 54
Gunners wakijiuliza baada da ya Reading kusawazisha bao
Kikosi cha Reading kikipanga jinsi ya kufanya Wembley usiku huu dhidi ya Arsenal
VIKOSI:Arsenal: Szczesny, Debuchy, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Coquelin, Ramsey, Cazorla, Ozil, Alexis, Welbeck
Akiba: Ospina, Gabriel, Monreal, Flamini, Wilshere, Walcott, Giroud
READING:
Federici, Gunter, Obita, Pearce, Hector, Williams, Chalobah, McCleary, Robson-Kanu, Mackie, Pogrebnyak
Akiba: Anderson, Kelly, Cooper, Karacan, Norwood, Cox, Yakubu
0 maoni:
Chapisha Maoni