Mshambuliaji
wa klabu ya Liverpool, Daniel Sturridge amefanyiwa upasuaji, akiwa
Nchini Marekani kwa lengo la kumaliza tatizo la majeraha ya paja ambayo
yamemsababishia kuwa nje ya uwanja katika kipindi hiki cha kuelekea
mwishoni mwa msimu wa 2014-15. Sturridge yupo nchini Marekani tangu Ijumaa lililopita na amewathibitishia hilo mashabiki kwa kuweka picha kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.
Inaaminika kwamba hatua ya kufanywa kwa upasuaji huo, itamuwezesha Sturridge kuwa katika hali nzuri ya kucheza kwa kujiamini kuanzia mwanzoni mwa msimu huu, baada ya kupata wakati mgumu katika kipindi cha msimu huu.
0 maoni:
Chapisha Maoni