
kwenye Fainali ya Mchujo wa Timu 4 za Daraja la Championship iliyochezwa Uwanjani Wembley Jijini London.
Mbele ya Watazamaji 85,656, Norwich City walipiga Bao zao 2 ndani ya Robo Saa ya Kwanza kwa Bao za Cameron Jerome alietumia vyema makosa ya Daniel Ayala na kufunga na kisha katika Dakika ya 15 Nathan Redmond alipiga Bao la Pili.


Norwich City sasa wameungana na Bournemouth na Watford, ambazo zilimaliza Nafasi mbili za juu za Ligi ya Championship na kupanda Daraja moja kwa moja, kucheza Ligi Kuu England Msimu ujao kuzibadili Hull City, QPR na Burnley zilizoporomoka Daraja.















0 maoni:
Chapisha Maoni