.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumapili, 31 Mei 2015

NAPOLI 2 vs 4 LAZIO,

By: Unknown On: Jumapili, Mei 31, 2015
  • Share The Gag

  • Marco Parolo dakika ya 33 kipindi cha kwanza aliifungia bao Lazio.

    Dakika ya majerhi ya kipindi cha kwanza Antonio Candreva alichomoka na kuwakacha mabeki na  kuwaliwafungia bao dakika ya 45 na kufanya 2-0 dhidi ya Napoli inayoongozwa na Rafael Benitez na kwenda mapumziko ikiwa nyuma ya bao mbili.

    Kipindi cha pili dakika ya 55 Gonzalo Higuaín aliifungia bao Napoli na kufanya 2-1 na mtanange kuanza kuchangamka.

    Lazio walicheza pungufu 10 uwanjani baada ya mwenzao kuoneshwa kadi nyekundu  na baadae Napoli dakika ya 64 Gonzalo Higuaín alisawazisha bao tena na kufanya 2-2.

    Nao Napoli dakika 70 mwenzao Faouzi Ghoulam alioneshwa kadi ya pili ya njano na kisha kuondoshwa kwa kadi nyekundu hivyo kucheza kila Timu wakiwa 10. 

    Dakika ya 75 Napoli walipata penati ya kizushi  na ya Utata na Gonzalo Higuaín kuikosa penati hiyo kwa kupaisha sana mpira juu ya lango la Lazio.

    Dakika ya 85 Ogenyi Onazi wa Lazio aliwamaliza Napoli nguvu pale alipowafunga bao kimaajabu na kuwapa  bao la 3 Lazio.
    Zikiwa zimeongezwa dakika 5 Lazio walipata tena bao la nne baada ya kupigwa frii kiki na M. Klose kuumalizia mpira huo nyavuni baada ya beki wao Napoli kupitwa.
    Na mtanange kumalizika kwa Lazio kuwa washindi wa bao 4-2 dhidi ya Napoli inayoongozwa na Rafael Benitez.

    Napoli wamemaliza msimu wakiwa nafasi ya 5 wakiwa na pointi 63 huku Lazio wakiwa nafasi ya tatu wakiwa na pointi 69.

    Rafael Benitez anaagwa na Napoli kwa kichapo cha bao 4-2 kutoka kwa Lazio huku kukiwa na fununu kwa asilimia kubwa kwa Kocha huyo kuhamia Klabu kubwa ya Spain ya Real Madrid kwenda kuwa mkufunzi wao kwa msimu huu unaokuja wa 2015/16.

    RAIS WA TANZANIA AONGOZA MKUTANO WA PILI WA DHARURA WA WAKUU WA NCHI WA EAC KUHUSU BURUNDI

    By: Unknown On: Jumapili, Mei 31, 2015
  • Share The Gag


  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa kwanza kulia) kwa pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museven (wa pili kulia), Rais wa Afrika Kusini, Mhe Jacob Zuma (wa tatu kutoka kulia), Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Alain Nyamitwe (wa tatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera (wa pili kushoto), wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili hali ya siasa na usalama nchini Burundi. Mkutano huo ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2015.

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (wa pili kutoka kulia) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Joyce Mapunjo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje (kulia) nao wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

    Dkt. Richard Sezibera akisoma maazimio yaliyofikiwa mara baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumalizika.

    Kundi la Watu Maalum la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalofuatilia hali ya siasa na usalama nchini Burundi chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba wakifuatilia mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini.


    Juu na Chini ni Wajumbe mbalimbali wakifuatilia mkutano wa wakuu wa nchi wa EAC

    Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. Radhia Msuya (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi Msaidizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi, Bibi Victoria Mwakasege nao wakifuatilia mkutano

    Maafisa Mambo ya Nje nao wakifuatilia kwa makini mkutano

    Sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini nao wakifuatilia mkutano

    Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene (katikati) kwa pamoja na Afisa Habari wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu Bw. Macdonald Mwakasendile (kushoto) wakirekodi matukio

    Rais Kikwete akifuraia jambo na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Zuma pamoja na Rais wa Uganda Mhe. Museveni mara baada ya kumaliza mkutano.

    Rais Kikwete akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bi.Nkoosazana Dlamini-Zuma kabla ya kuanza mkutano.

    Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiongozana na Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta tayari kwenda kuanza mkutano wa kujadili hali ya usalama nchini Burundi .

    Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula akizungumza jambo na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya,, Bw. Vervaeke.
    ....Kuwasili kwa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

    Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Mulamula akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta




    Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyetta akipita kwenye Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili nchini



    Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Harrison Mwakyembe akimtambulisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula kwa Rais wa Uganda mara baada ya kumpokea Rais huyo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

    Rais Museven akipita katikati ya Gwaride la heshima.

    Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Balozi Radhia Msuya akisalimiana na Rais wa Afrika ya Kusini alipowasili nchini

    Picha ya Pamoja baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

    MH. MWIGULU NCHEMBA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS MKOANI DODOMA

    By: Unknown On: Jumapili, Mei 31, 2015
  • Share The Gag


  • Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akiwapungia mkono baadhi ya wafuasi wake waliojitokeza kwa wingi,kumsikiliza wakati akitamka kutangania nia ya kugombea kiti cha uraui kupitia CCM.


    Baadhi ya wakazi wa Dodoma wakimsikiliza kwa makini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alipokuwa akitangaza nia yake ya kugombea kiti cha Urais kupitia chama cha CCM

    Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Dodom mapema jioni ya leo katika moja ya ukumbi wa chuo cha Mipango

    Baadhi ya wakazi wa Dodoma wakimsikiliza kwa makini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alipokuwa akitangaza nia yake ya kugombea kiti cha Urais kupitia chama cha CCM

    VIJANA WA KAWE WASHIRIKI JOGGING

    By: Unknown On: Jumapili, Mei 31, 2015
  • Share The Gag


  • Vijana wa Kawe wakishiriki Jogging.

    Gabriel Munasa (mwenye kaptura ya pink) akishiriki jogging pamoja na vijana wa Kawe,kushoto kwake ni Elias Nawera.






    Bendera ya Taifa ikiwa juu kuashiria kuhitimisha kwa mchakamchaka huo ambao mgeni rasmi alikuwa Gabriel Munasa.

    Gabriel Munasa akishiriki mazoezi ya viungo kwenye viwanja vya michezo vya Kawe.

    RAFAEL BENITEZ NJIA NYEUPE KUTUA REAL MADRID, MAKAMU WA REAL AWEKA WAZI!

    By: Unknown On: Jumapili, Mei 31, 2015
  • Share The Gag


  • Makamu Rais wa Real Madrid ameropoka na kutamka kuwa Rafael Benitez ndie Kocha Mkuu wao mpya.
    Benitez anatarajiwa kuachia ngazi kwenye Klabu yake ya sasa Napoli ya Italy mara baada ya kumaliza Mechi yao ya mwisho ya Msimu wa Serie A Leo hii Jumapili.
    Lakini, Makamu Rais wa FIFA, Eduardo Fernandez de Bla, akiongea kwenye Kikao cha Mashabiki wa Real hapo Jana, alisema: " Carlo Ancelotti Kocha Bora Duniani kama alivyokuwa Jose Mourinho Miaka Miwili iliyopita na kuanzia Wiki hii, Benitez ndie atakuwa Kocha Bora! "
    Wiki iliyopita Real ilimtimua Ancelotti baada ya Msimu huu kutwaa Taji moja tu, Kombe la Klabu Bingwa Duniani, wakati Msimu uliopita walibeba Kombe la Klabu Bingwa Ulaya na Copa del Rey.
    Nae Mourinho, ambae sasa ni Bosi wa Chelsea, alifukuzwa na Real 2013 baada ya kutwaa Ubingwa wa La Liga na Copa del Rey, mara moja moja, katika himaya yake ya Miaka Mitatu.
    Benitez, Raia wa Spain mwenye Miaka 55, aliiongoza Liverpool kutwaa UEFA CHAMPIONS LIGI Mwaka 2005 na kutwaa EUROPA LIGI na Chelsea Mwaka 2013 na kisha kujiunga na Klabu ya Italy, Napoli, ambayo alitwaa nayo Coppa Italia Mwaka 2014.
    Kocha huyo pia aliweza kutwaa Ubingwa wa La Liga mara 2 na UEFA CUP mara moja wakati akiwa na Valencia kati ya Mwaka 2001 na 2004.
    Kati ya Mwaka 1993 na 1995 alifundisha Kikosi cha Akiba cha Real Madrid.Rafael Benitez

    STARTIMES KUANZA KUONYESHA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA U20

    By: Unknown On: Jumapili, Mei 31, 2015
  • Share The Gag

  • Na Dotto Mwaibale
    WAPENZI wa soka nchini sasa watafaidi kwa kutazama michuano ya kombe la dunia chini ya miaka 20 mwaka 2015 moja wa moja kwenye luninga zao kupitia ving’amuzi vya StarTimes pekee.
    Michuano hiyo ambayo itaanza kutimua vumbi tarehe 30 mwezi Mei na kumalizika tarehe 20 mwezi Juni mwaka huu moja kwa moja kutoka nchini New Zealand ambapo timu 24 za vijana kutoka mataifa mbalimbali duniani yatachuana kuwania ubingwa.
    Akizungumza baada ya kupata haki miliki kutoka kwa FIFA za kutangaza michuano hiyo maarufu duniani ambayo hubeba mastaa wa baadae kwa timu zao za taifa, Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amesema kuwa wanafuraha kubwa kuonyesha michuano hiyo kwani soka ni mchezo unaopendwa zaidi duniani.
    “Tunayofuraha kubwa kuwatangazia wateja wetu kuwa tumepata haki miliki kutoka FIFA za kuonyesha michuano ya kombe la dunia kwa vijana wa umri chini ya miaka 20 mwaka 2015 itakayofanyika nchini New Zealand. Soka ni mchezo unaopendwa zaidi nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla na tunaamini tutawapatia wateja wetu burudani ya matangazo yenye ubora wa hali ya juu kupitia ving’amuzi vya StarTimes.” Alisema Bi. Hanif

    PSG WASHEREKEA UBINGWA WAO WA 2015 BAADA YA KUITANDIKA 1-0 AUXERRE

    By: Unknown On: Jumapili, Mei 31, 2015
  • Share The Gag


  • Waliifunga bao 1-0 Timu ya AuxerreEdinson Cavani ndiye aliyeitungua bao la pekee la kichwa Timu ya AuxerreCavani akipongezwaPSG wakiungana kushangilia na kuwapongeza Mashabiki waoMashabiki wakiitikia kwa wingi!Zlatan Iblahimovic akishikilia Kombe laoThiago Silva na Zlatan pamojaMakombe yao juu