.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumamosi, 28 Februari 2015

TUZO ZA WASANII BORA WA MUZIKI WA ZANZIBAR MWAKA 2015

By: Unknown On: Jumamosi, Februari 28, 2015
  • Share The Gag
  • Mkurugenzi wa Biashara Zanzibar Nd. Mohamed Baucha wa kulia akimkabidhi Tunzo ya Video bora ya mwaka muziki wa kizazi kipya Nassir Hassan (Vanila) mara baada ya kuibuka mshindi, tunzo hizo zimeandaliwa na Kampuni ya Zanzibar Media Corporation LTD katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Zanzibar.
    Mwanamitindo marufu wa Zanzibar Farouk Abdillahi…
    Mkurugenzi wa Biashara Zanzibar Nd. Mohamed Baucha wa kulia akimkabidhi Tunzo ya Video bora ya mwaka muziki wa kizazi kipya Nassir Hassan (Vanila) mara baada ya kuibuka mshindi, tunzo hizo zimeandaliwa na Kampuni ya Zanzibar Media Corporation LTD katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Zanzibar.
    Mwanamitindo marufu wa Zanzibar Farouk Abdillahi akimkabidhi Tunzo ya Video bora mwaka ya Taraab Bi. Saada Nassor.
    Meneja wa Zenji Entertainment Seif Moh'd (kushoto) akimkabidhi tunzo Mwanamuziki Bora wa kiume wa tarabu asili Cholo Ganun.
    Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Dkt. Mwinyihaji Makame akimkabidhi tunzo ya muandaaji bora wa Tamasha Zanzibar Music Award mwaka 2015 Mbunge wa Jimbo la Uzini na Mkurugenzi wa Redio ya Zenji FM Mohamed Seif Khatib katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Holl Bwawani Mjini Zanzibar.
    Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Dkt. Mwinyihaji Makame katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Zanzibar Midia Corporation LTD. Picha zote na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.

    BLOGGERS KUKUTANA KESHO KATIKA HOTELI YA SERENA JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA PATI YA KIHISTORIA

    By: Unknown On: Jumamosi, Februari 28, 2015
  • Share The Gag


  • Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na mmiliki wa Blog ya The Habari.com Joachim Mushi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi. Kutoka kushoto ni mjumbe wa TBN Mkala Fundikira, Afisa wa kampuni ya mawasiliano na matangazo ya AIMS, Shafiq Mpanja wa AIM, Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale na mjumbe wa TBN Khadija Kalili.
    Katika mkutano huo TBN imesema kesho Jumamosi jioni Bloggers takriban 100 kutoka sehemu mbalimbali Nchini watakutanika katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es salam kwa ajili ya hafla ya mwaka mpya itayohudhuriwa pia na wadhamini na marafiki wa Bloggers.

    Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo wakati wa mkutano.

    Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili akizungumza wakati wa mkutano.

    Father Kidevu (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano.
    Baadhi ya Bloggers na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari Maelezo Dar es Salaam.

    MANCHESTER UNITED KUCHEZA NA SUNDERLAND OLD TRAFFORD

    By: Unknown On: Jumamosi, Februari 28, 2015
  • Share The Gag


  • Manchester United captain Wayne Rooney speaks with Jonny Evans ahead of the game at Old Trafford
    Kepteni wa Manchester United Wayne Rooney akiteta jambo na Jonny Evans juu ya Mchezo huo ambao wote wamepeana hamasa ya kuibuka na Ushindi kesho dhidi ya Sunderland.Radamel Falcao trains at Carrington as Manchester United prepare to play Sunderland in the Premier League at Old Trafford
    Radamel Falcao akijifua kwenye Uwanja wa Carrington, Manchester United wakijiandaa kuikaribisha Sunderland ngland, Premier League mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford
    Louis van Gaal admits he doesn't know when Dutch striker Robin van Persie will return to action
    Meneja Louis van Gaal amezungumza ila hakuweka wazi juu Robin van Persie atakaa nje muda gani ila amesema ni wiki kadhaaVan Gaal
    Robin van Persie leaves the Liberty Stadium on crutches and with his right leg in a protective boot 
    Robin van Persie  aliumia wiki iliyopita wakati  wa Mchezo wao na Swansea City huko kwenye Uwanja wa Liberty, Aliumia Enka.

    Michezo mitano ijayo ya MANCHESTER UNITED
    February 28: Sunderland (nyumbani)
    March 4: Newcastle (Ugenini)
    March 9: Arsenal (Nyumbani)
    March 15: Tottenham (Nyumbani)
    March 22: Liverpool (Ugenini)
    Van Gaal speaks to the media during a press conference ahead of United's game against Sunderland
    Van Gaal akiteta kwenye Vyombo vya Habari juu ya mchozo wao na  Sunderland kesho jumamosi 28
    Goalkeepers David de Gea (left) and Victor Valdes (right) in action during a training session on Friday
    Makipa: David de Gea na Victor Valdeswakiteta jambo hii leo wakati wa mazoezi
    Luke Shaw (left) and Juan Mata (right) are expected to line up against the Black Cats at Old Trafford
    Luke Shaw na Juan Mata wote wanategemewa kucheza mchezo wao wa kesho Old Trafford dhidi ya Sunderland
    Marcos Rojo (left) warms up as team-mates Daley Blind and Wayne Rooney observe
    Marcos Rojo na Daley Blind pamoja na Wayne Rooney kesho kuonesha makeke yao

    Van Pesrsie aliumia wakati wa Mchezo na Swansea City walipopewa kichapo cha bao 2-1

    Ijumaa, 27 Februari 2015

    RATIBA LIGI KUU ENGLAND WIKIENDI HI JUMAMOSI FEB, 28 NA JUMAPILI

    By: Unknown On: Ijumaa, Februari 27, 2015
  • Share The Gag

  • www.bukobasports.comLIGI KUU ENGLAND
    RATIBA
    Jumamosi Februari 28

    15:45 West Ham v Crystal Palace
    18:00 Burnley v Swansea
    18:00 Man United v Sunderland
    18:00 Newcastle v Aston Villa
    18:00 Stoke v Hull
    18:00 West Brom v Southampton

    Jumapili Machi 1
    15:00 Liverpool v Man City
    17:05 Arsenal v Everton

    Alhamisi, 26 Februari 2015

    Tanzania kushiriki mashindano ya kuogelea kanda ya 4

    By: Unknown On: Alhamisi, Februari 26, 2015
  • Share The Gag


  • photos.demandstudios.com-getty-article-197-91-87788991_XS
    Na Amplifaya Amplifaya
    KOCHA wa timu ya Taifa ya Kuogelea, Alex
    Mwaipasi amesema Tanzania inatarajiwa
    kushiriki kwenye mashindano ya Kanda ya Nne
    yaliyopangwa kufanyika nchini Angola, Mei
    mwaka huu.
    Mara ya mwisho mashindano hayo kufanyika
    ilikuwa ni mwaka jana nchini Uganda ambapo
    Tanzania iliwakilishwa na wachezaji kadhaa
    waliofanya vizuri wakiwamo Hilal Hilal na Sonia
    Tomiotto.
    Akizungumza jana, Mwaipasi
    alisema katika kuhakikisha wanafanya vizuri
    katika mashindano ya mwaka huu, tayari
    wameshaanza mchakato wa kusaka kikosi bora.
    “Tumeanza mchakato wa kuwatafuta wachezaji
    bora kutoka mikoa ya Mwanza, Arusha,
    Morogoro na Dar es Salaam na tuna imani
    mambo yatakuwa mazuri tutakapoanza kambi
    baadaye,” alisema Mwaipasi.
    Alisema wachezaji hao watafuatiliwa mwenendo
    wao katika mashindano ya kitaifa
    yatakayofanyika mwezi ujao, na mashindano ya
    wazi ya Afrika yatakayofanyika nchini Afrika
    Kusini.

    Kipa wa Yanga kutimkia Ligi Kuu ya India

    By: Unknown On: Alhamisi, Februari 26, 2015
  • Share The Gag

  • jUMA MPONGO 1Na. Richard Bakana, Dar es salaam
    MLINDA mlango wa zamani wa klabu ya Dar es salaam Young Africans (Yanga SC)  ambaye kwa sasa anakipiga kunako ligi kuu ya nchini Oman (Omantell Professional League) ndani ya  Al Seeb Club, Juma Mpongo huenda akalamba shavu la kusakata kabumbu katika ligi kuu ya India.
    Akizungumza na Shaffihdauda.com akiwa Oman, Mpongo ambaye amewahi kuzichezea timu za Tanzania prisons, Twiga sports, Coastal Union na Ashanti United, amesema kuwa mchakato wa kutimkia India upo kwenye njia na hiyo imekuja baada ya kuwepo na fununu za kutaka kuzuia magolikipa kutoka nje ya Oman kucheza ligi za nchi hiyo. 
    “Kwa kiasi flani naweza sema ndoto zangu zimetimia, lakini bado nina ndoto ya kupata challenge nyingine, Pia bado napambana ili niende mbele zaidi kadiri Mungu atakavyo niwezesha, Kama mipango inaenda vizuri naweza kuhamia ligi kuu ya India, Mipango inaendelea kaka, bado sijaambiwa ni Timu gani kwa sasa, Hapa inawezekana sheria zikabadirika baada ya msimu huu kumalizika, Kuna tetesi msimu ujao wanaweza kufuta kuingiza Magolikipa kutoka nje ya nchi hii” Amesema Juma Mpongo ambaye timu yake ya mwisho kuichezea Tanzania ni Ashanti United iliposhuka daraja mwaka jana. JUMA MPONGO 2
    Mpongo ambaye pia amewahi kucheza soka la kulipwa nchini Congo kunako klabu ya DC Virunga, na Rwanda katika timu za Kiyovu sports na Rayon sports, amezungumzia kwa ujumla Maisha ya mpira Oman na tofauti iliyopo kati ya Soka la Tanzania na kwa waarabu hao ambapo ametililika kama hivi. 
    “Maisha ya huku sio mepesi sana kama ambavyo tunafikiria japo ugumu upo tena mkubwa tu, Tofauti kwenye soka sio kubwa Sana, Lakini huku wenzetu kila kitu wanacho pia kuna mashindano Mengi ambayo yanamfanya mchezaji awe bize muda wote, Ligi inaushindani Mkubwa sana, huwezi amini kaka, sisi tumecheza mechi 6 ndani ya siku 11 mashindano tofauti” Amesema Mpongo ambaye timu yake ya Al Seeb inashika nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 13 huku kinara wa ligi hiyo akiwa na alama 32.juma mpongo
    Alituaje Oman? 
    Kipa huyo ambaye ni mzaliwa wa Nzega mkoani Tabora, ametoboa siri ya kupata nafasi ya kukipiga Oman na kusema kuwa, mlinda mlango wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Peter Manyika ambaye ndio mwalimu wake aliyekuwa akimnoa katika kituo chake cha makipa kilichopo Karume Jijini Dar es salaam, baada ya kuridhishwa na kiwango chake akaamua kumpatia ulaji huo na kuwaacha wakongwe kama Juma Kaseja akibakia Tanzania. 
    “Kwa kweli nafasi hii nilipewa na aliyekuwa kocha wa Makiipa wa Timu hii msimu uliopita, Coach Peter Manyika, Aliona uwezo wangu kwani nilikuwa nafanya mazoezi katika kituo anachokiendesha hapo Dar uwanja wa Karume ndipo akavutiwa na mimi, Ni kweli tulikuwa wote pale kituoni mimi, Kaseja na wengineo na wao bado wanaendelea” Amesema Juma Mpongo ambaye unaweza kumuita Baba Halidi.
    Kuhusu familia yake, Je, anaishi nayo Oman?
    Mlinda mlango huyo namba moja wa klabu ya Al Seeb, amesema kuwa licha kuwa na majukumu ya kuhakikisha analinda lango la timu yake isivamiwe na wapinzani, lakini bado anamajukumu ya kulea familia yake ya Watoto watatu, pamoja na mke mmoja, licha ya kuwa mbali nao akimaanisha kuwa Familia yake ipo Dar es salaam.
    “Familia yangu ipo Dar es salaam kaka, Namshukuru Mungu Nina Watoto watatu wote wakiume, Wa kwanza anaitwa Halidi Juma Mpongo huyu ana umri wa Miaka 10 sasa, Wa pili anaitwa Mohamed Juma Mpongo ana umri wa miaka 7 sasa na Wa tatu ambaye Ndio mdogo anaitwa Rahim Juma Mpongo ana umri wa Miaka 5,  Wote wa napenda Sana soka ila huyu mdogo yeye huwa anataka hadi gloves zangu nimpe” Amefunguka Juma Mpongo. JUMA MPONGO MTOTO
    Kuna Watanzania wengine wanao cheza Oman?
    “Kwenye ligi kuu ni Mimi peke yangu ila madaraja ya chini yupo Thomas moris ila sijajua anacheza Timu gani na daraja gani kwani Timu yao ipo nje kabisa ya Muscat” Amesema Baba Halidi. 
    Ushauri wake kwa wachezaji na TFF 
    “Cha msingi ni kujituma na kufanya kazi kwa bidii kwa Magolikipa mwenzangu, pia TFF na wadau wote wa soka tupambane ili kuinua soka la nchi yetu maana bado tuko chini, na ligi yetu iendeshwe kwa msingi ya haki zaidi ili bingwa anaepatikana aweze kutuwakilisha vizuri kimataifa, TFF iandae mashindano mengine ili wachezaji wasiwe wanakaa muda mrefu bila kucheza, kuwepo na vikombe, kwa mfano hapa Oman, kuna kumbe linaitwa Mazda cup Hili limeandaliwa kwa ajili ya kufanya wachezaji wasikae muda mrefu bila kucheza pindi Timu ya taifa inapokuwa na majukumu ya Kimataifa, Hayo Ndio maono yangu kaka” Amefunga kazi  mtu mzima Baba Rahim.
    MWISHO.JUMA MPONGO 3JUMA MTOTO

    Yanga waipashia BDF XI …Azam TV sasa kuonyesha mechi ni ‘Laivu’ !!

    By: Unknown On: Alhamisi, Februari 26, 2015
  • Share The Gag


  • IMG-20150226-WA0005
    Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi Botswana leo
    WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho, Dar Young Africans wameendelea na mazoezi ya mwisho mwisho nchini Botswana kujiandaa na marudiano dhidi ya wenyeji BDF XI itayopigwa kesho kutwa, februari 28 mwaka huu.
    Yanga chini ya kocha mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm wapo katika morali ya ushindi na wachezaji wote waliosafiri wapo salama.
    IMG-20150226-WA0006
    Bahati nzuri kwa Yanga ni kwamba wataingia uwanjani wakiwa na faida ya mabao 2-0 waliyovuna uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, februari 14 mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
    Mabao yote siku hiyo yalifungwa na Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe.
    Ili kusonga mbele Yanga wanahitaji ushindi, suluhu au sare ya aina yoyote ile au wasifungwe zaidi ya goli 1-0.
    IMG-20150226-WA0007
    Kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm (kushoto) baada ya mazoezi akiwa ameketi na nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwenye basi walilotumia kutoka Hotelini kwenda uwanjani.
    Habari njema kwa wapenzi wa soka nchini ni kwamba mtanange huo utaoneshwa moja kwa moja ‘Live’ kipitia kituo cha Televisheni cha Azam TV kuanzia majira ya saa 2:30 usiku.
    Mechi ya kwanza Dar es salaam, Yanga walipiga marufuku chombo chochote cha TV kuonesha mechi hiyo, lakini safari matangazo yatapokelewa na Azam TV moja kwa moja kutoka Botswana  na kuwafikia Watanzania wote.

    Alichokisema Pluijm kuelekea mechi ya Yanga kesho Botswana

    By: Unknown On: Alhamisi, Februari 26, 2015
  • Share The Gag

  • pluijm
    Na Bertha Lumala
    Kocha mkuu wa Yanga SC, Hans van der Pluijm amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanatikisa nyavu za wapinzani wao BDF XI FC katika mechi yao ya kesho ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
    Yanga SC, mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara, watakuwa na kibarua kigumu mbele ya wenyeji wao hao watakapopamba katika mechi hiyo ya marudiano ya hatua ya awali ya michuano itakayochezwa kuanzia saa 2:00 usiku Uwanja wa SSKB Lobatse uliopo Km 70 kutoka Gaborone, mji mkuu wa Botswana. Uwanja huo upo kwenye kambi ya Jeshi la Ulinzi (BDF) eneo la Lobatse, Botswana.
    Katika mahoajino na mtandao huu akiwa Botswana leo mchana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Jerry Muro amesema benchi lao la ufundi linaloongozwa na Pluijm limewataka wachezaji kuhakikisha wanapata japo goli moja la ugenini huku wakilinda mabao yao mawili waliyofunga nyumbani.
    “Tulishinda 2-0 nyumbani, lakini kocha (Pluijm) amewataka wachezaji kutobweteka na ushindi huo. Amesema ni lazima tusakae japo goli moja la ugenini ili tuwe salama zaidi huku tukihakikisha wenyeji wetu hawapati mabao,” amesema Muro.
    Pluijm amesema ushindi wa timu hiyo kwenye mechi za Ligi Kuu ni chachu kuelekea mchezo huo wa marudiano dhidi ya BDF
    Aidha, mitandao ya michezo ya Botswana imemnukuu Pluijm akitamba kupata ushindi mwingine wakati timu hizo zitakaporudiana kesho.
    Pluijm amekaririwa akieleza kuwa, licha ya kucheza ugenini, bado ana uhakika watawafunga wenyeji wao BDF XI FC katika mchezo huo.
    “Tumekuja Botswana kucheza kwa kushambulia kama tulivyofanya nyumbani tuliposhinda mabao 2-0, ninajua mchezo utakuwa mgumu kwa sababu wanacheza kwao na watataka kutushambulia, lakini sisi tutacheza kwa malengo huku tukihitaji bao moja ili kuwapa presha wenyeji,” amesema Pluijm.
    Pluijm amesema ushindi wa timu hiyo katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ni chachu kuelekea mchezo huo wa marudiano dhidi ya BDF na kuwataka mashabiki kuiunga mkono timu yao kuelekea mechi hiyo.
    Hata hivyo, mashabiki wa Yanga SC waliokuwa wasafiri kwa basi kubwa la klabu hiyo Jumatano alfariji, walikwama kutokana na kile kilichoripotiwa leo kuwa basi hilo halina bima wala kibali cha barabarani.
    Yanga SC ambayo kwa muda mrefu imekuwa haifiki mbali katika michuano ya kimataifa ikitolewa kwa matuta dhidin ya Al Ahly ya Misri katika hatua ya pili mwaka jana, inahitaji sare ya aina yoyote au kipigo kisichozidi bao 1-0 kusonga mbele.
    Endapo timu hiyo ya Jangwani ikifanikiwa kuwang’oa maafande hao, itakutana na mshindi kati ya Sofapaka FC ya Kenya na Platnum FC katika hatua inayofuata. Wazimbawe walishinda 2-1 dhidi ya Sofapaka katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Nairobi wiki mbili zilizopita.

    Jumatano, 25 Februari 2015

    UEFA CHAMPIONS LEAGUE: ARSENAL 1 vs 3 AS MONACO,

    By: Unknown On: Jumatano, Februari 25, 2015
  • Share The Gag

  • 2-0 Bao la pili la As Monaco lilifungwa na Berbatov dakika ya 53 na kuwaacha Arsenal wakiduwaa.2-0Emirates!!Ooops ..3-1Watajutaa!!
    Muuaji wa bao la tatu Yannick Ferreira Carrasco. Kipa wa Arsenal David Ospina akiwa hoi baada ya kushonwa baoFuraha ya Ushindi Ugenini!! 3-1Kiongozi Prince  Albert akishangilia Ushindi mwishoni!! Baada ya timu ya As Monaco kuitoa kamasi Arsenal.Olivier Giroud akiwa hana hamu na kipute!
    Hoi!! Hakuna cha Sanchez!!Hali tete!!2-1Alex Oxlade akishangilia baada ya kurudisha bao moja Baadhi ya Wachezaji wa Arsenal wakipagawa baada ya kufungwa na As Monaco
    Kipindi cha pili dakika ya 53 Dimitar Berbatov aliwachoma bao la pili Arsenal na kufanya 2-0 dhidi ya Arsenal. Dakika ya 90 kwenye dakika za najeruhi Alex Oxlade-Chamberlainaliwapachikia bao lao la pekee lakini Yannick Ferreira Carrasco aliyeingia kipindi cha pili alimaliza mchezo kwa kufunga bao la tatu na kufanya 3-1 na mtanange kumalizika.
    Geoffrey Kondogbia salamu salaam akituma!!Arsenal hoi!!Kimagumashi tuu As Monaco wameichakaza Arsenal kwao!Geoffrey Kondogbia akishangilia bao lake baada ya kuichapa bao Arsenal katika dakika ya 38.
    Prince Albert was in attendance to watch his beloved Monaco take a giant step toward reaching the quarter-finals of the competition
    Prince Albert nae alikuwemo kipenzi cha Monaco..kwenye uwanja wa Emirates usiku huu!
    The travelling fans were in good voice all night, with Monaco giving their supporters much to cheer about on the pitch
    Mashabiki walisafiri kuja kuipa kampani ya Nguvu timu yao As Monaco kwenye Uwanja wa Emirates!!
    A Monaco fan holds up a sign acknowledging the work of Arsene Wenger and Eric Di Meco for the French club
    Mashabiki wa Monaco na Ujumbe wao!! Shukrani zao!!
    Geoffrey Kondogbia aliifungia bao dakika ya 38 kipindi cha kwanza na kufanya As Monaco kuongoza kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Arsenal katika kipindi cha kwanza. Baada ya Per Mertesacker kuugusa mpira na kuuhamisha uelekea kwa kipa wake David Ospina langoni. Hadi mapumziko Arsenal 0-1 As Monaco.Kikosi kilichoanza cha ArsenalAlex SanchezGeofrey akichuana na Cazorla Kondogbia akiachia shuti kali1-0BaoKipa wa Monaco Danijel akipagawa kwa furaha kwa kuruka juu baada ya timu yake kushindaPongezi!!Wacezaji As Monaco wakipongezana Mtatukomaa!! Viongozi nao wa Monaco yale yale...full mzukaaa...Kocha wa As Monaco Leonardo Jardim Ni Arsenal vs AS Monaco
    VIKOSI:
    Arsenal:
    Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Coquelin, Cazorla, Sanchez, Ozil, Welbeck, Giroud.
    Akiba: Szczesny, Gabriel, Rosicky, Walcott, Oxlade-Chamberlain, Monreal, Chambers.
    Monaco: Subasic, Toure, Wallace Santos, Abdennour, Echiejile, Dirar, Kondogbia, Fabinho, Joao Moutinho, Martial, Berbatov.
    Akiba: Stekelenburg, Kurzawa, Matheus Carvalho, Bernardo Silva, Carrasco, Alain Traore, Diallo.
    Refa: Deniz Aytekin (Germany)