.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumamosi, 25 Februari 2017

DABI DAR: SIMBA 2 vs 1 YANGA.

By: Unknown On: Jumamosi, Februari 25, 2017
  • Share The Gag

  • Image may contain: 2 people, stadium and outdoorDabi ya Kariakoo uliochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Leo ulishuhudia Mtu Simba ikitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa Yanga 2-1.
    Yanga walifunga Bao lao Dakika ya 5 kwa Penati ya Simon Msuva iliyotolewa baa Fowadi wao Obrey Chirwa kuangushwa na Beki Novatus Lufunga.

    Image may contain: 8 people, people standing, stadium, grass and outdoorDakika ya 55 Simba walibaki Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Janvier Besala Bokungu kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kulambwa Kadi za Njano 2.
    Simba wakasawazisha Bao Dakika ya 66 kupitia Laudit Mavugo aleingizwa Kipindi cha Pili na kufunga Bao la Pili na la ushindi Dakika ya 81 Mfungaji akiwa Shiza Kichuya.
    VPL, inayoshirikisha Timu 16, sasa inaongozwa na Simba wenye Pointi 54 kwa Mechi 23 na Yanga ni wa Pili wakiwa na Pointi 49 kwa Mechi 22 huku Azam FC ni wa 3 wakiwa na Pointi 41 kwa Mechi 23.
    VIKOSI:
    SIMBA:
    Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga [Shiza Kichuya, 51’], Abdi Banda, James Kotei, Ibrahim Hajib, Muzamil Yassin, Juma Luizio [Said Ndemla, 27’], Laudit Mavugo, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim [Jonas Mkude, 57’].

    YANGA:
    Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Andrew Vincent, Kevin Yondan, Justine Zulu [Juma Mahadhi, 78’], Simoni Msuva, Thabani Kamusoko [Said Juma ‘Makapu’, 45’], Amisi Tambwe [Deus Kaseke, 70’], Obrey Chirwa, Haruna Niyonzima.

    REFA:
    Mathew Akrama [Mwanza]
    WASAIDIZI: Mohammed Mkono [Tanga] na Hassan Zani [Arusha]

    Jumanne, 21 Februari 2017

    Ukimuuliza Jose Mourinho kama Wayne Rooney anaondoka Man United

    By: Unknown On: Jumanne, Februari 21, 2017
  • Share The Gag


  • Kocha wa Man United Jose Mourinho kuelekea mchezo wao wa marudiano wa Europa League dhidi ya St Etienne ya Ufaransa, ameulizwa maswali kuhusu hatma ya nahodha wa Man United Wayne Rooney kama ataondoka katika timu hiyo au atabaki.
    Jose Mourinho ambaye inaaminika ndio anaweza akafanya Rooney aondoke mwisho wa msimu kama inavyoripotiwa au akabaki, ameshindwa kuweka wazi kama ataondoka staa huyo au atabaki, lakini amekiri kuwa hawezi kumlazimisha mchezaji kuhama.
    “Kuhusu kuondoka unaweza kumuuliza mwenyewe kwa sababu hata mimi siwezi kukuhakikishia kama nitakuwa hapa wiki ijayo, sasa nawezaje kukuhakikishia kuwa mchezaji ataendelea kuwepo msimu ujao, kama Rooney ataamua kuondoka sio kwa sababu mimi nataka aondoke”

    “Hicho ndio ninachoweza kukuhakikishia sitaweza kulazimisha legend wa Club hii kwenda sehemu nyingine, hivyo unaweza kumuuliza Rooney mwenyewe kama angependa kumaliza soka lake katika timu hii? lakini mimi nina furaha kuwa nae katika timu”

    Jumatatu, 13 Februari 2017

    RATIBA UEFA CHAMPIONS LEAGUE: JUMANNE NI BENFICA vs BVB, PSG vs BARCELONA, JUMATANO NI BAYERN vs ARSENAL, REAL MADRID vs NAPOLI

    By: Unknown On: Jumatatu, Februari 13, 2017
  • Share The Gag

  • UEFA CHAMPIONS LIGI
    Raundi ya Mtoano ya Timu 16 

    Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku
    Mechi za Kwanza
    Jumanne 14 Februari 2017

    Benfica v Borussia Dortmund
    Paris Saint Germain v Barcelona

    Jumatano 15 Februari 2017
    Bayern Munich v Arsenal
    Real Madrid v Napoli

    Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, inaanza Jumanne Usiku kwa Mechi mbili na Jumatano pia zipo Mechi mbili na kuendelea Wiki ijayo, zote zikiwa ni Mechi za Kwanza za Raundi hiyo.
    Jumanne ni huko Portugal wakati Benfica wakiikaribisha BVB Borussia Dortmund na nyingine ni huko Jijini Paris, Paris pale Paris Saint Germain wakicheza na Barcelona.
    Jumatano pia zipo Mechi 2 za Raundi hii ambapo huko Germany ni Bayern Munich na Arsenal na nyingine ni kule Santiago Bernabeu Jijini Madrid Nchini Spain kati ya Real Madrid na Napoli ya Italy.

    Mechi za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UCL zitakamilika Wiki ijayo, Jumanne na Jumatano kwa Mechi 4.

    Dondoo Muhimu:
    Benfica v Borussia Dortmund

    Mechi hii itachezwa huko Estádio do Sport Lisboa e Benfica, Lisbon na kuchezeshwa na Refa mzoefu kutoka Italy Nicola Rizzoli.
    Timu hizi zimekutana mara 2 Ulaya na kila moja kushinda mara moja.
    Benfica watatinga kwenye Mechi hii wakiwakosa Andrija Zivkovic, alie Kifungoni, na Majeruhi Lisandro Lopez huku Jonas akiwa kwenye hatihati kucheza kutokana na maumivu.
    Nao BVB watawakosa Majeruhi Mario Götze na Sven Bender huku hatihati ikiwa kwenye maumivu Nuri Şahin na Sebastian Rode.

    Paris Saint Germain v Barcelona
    Mechi hii ipo ndani ya Parc des Princes Jijini Paris Nchini France na itachezeshwa na Refa Szymon Marciniak kutoka Poland.

    Katika Mechi zilizopita, PSG ilishinda mara 2, Sare 3 na Barca kushinda 4 kati yao.

    PSG kwenye Mechi hii itamkosa Thiago Motta ambaye yupo Kifungoni wakati Barca watawakosa Majeruhi Arda Turan, Javier Mascherano na Aleix Vidal.

    UEFA CHAMPIONS LIGI
    Raundi ya Mtoano ya Timu 16

    Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku 
    Mechi za Kwanza
    Jumanne 21 Februari 2017

    Bayer 04 Leverkusen v Atlético Madrid
    Manchester City v Monaco

    Jumatano 22 Februari 2017
    FC Porto v Juventus
    Sevilla v Leicester City
     

    Mechi za Pili
    Jumanne 7 Machi 2017

    Arsenal v Bayern Munich
    Napoli v Real Madrid

    Jumatano 8 Machi 2017

    Barcelona v Paris Saint Germain
    Borussia Dortmund v Benfica


    Jumanne 14 Machi 2017
    Juventus v FC Porto
    Leicester City v Sevilla

    Jumatano 15 Machi 2017
    Atlético Madrid v Bayer 04 Leverkusen
    Monaco v Manchester City

    ANTONIO CONTE AMJIBU JOSE MOURINHO KIMYAKIMYA! 'SIPENDI MZAHA WA MOURINHO!"

    By: Unknown On: Jumatatu, Februari 13, 2017
  • Share The Gag

  • Antonio Conte amesema hapendi 'mzaha'wa Jose Mourinho baada ya Meneja huyo wa Manchester United kudai Chelsea ambao ni Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, hawawezi kukamatika kileleni kwa sababu ni Timu 'inayojihami mno!'.
    Hivi sasa Chelsea wapo Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Tottenham baada Jana kutoka 1-1 na Burnley huko Turf Moor.
    Mourinho, ambae anasifika kwa kuchota akili za Mameneja wapinzani na kuwavuruga, Juzi alidai Chelsea haiwezi kuteleza kutoka kileleni kwa vile 'wanajihami mno' na kushinda kwa kutumia 'kaunta ataki'.
    Jana Meneja wa Chelsea Antonio Conte alijibu mapigo kwa kusema: "Hiyo ni hadaa yake. Nina uzoefu kuelewa hilo!"
    Mara nyingi Mourinho amekuwa akikwaruzana na Mameneja wenzake kutokana na vijembe vyake vya kuwapandisha munkari ili kushinda vita ya kisaikolojia na muhanga mkuu wa mashambulizi hayo huko nyuma akiwa Arsene Wenger wa Arsenal.

    Hata hivyo Conte amegoma kuburutwa kwenye vita hiyo na kujibu: "Sipendi kujibu kuhusu Makocha wengine!" 

    EPL – Ligi Kuu England
    RATIBA:
    Jumatatu Februari 13

    2300 Bournemouth v Manchester City
    Jumamosi Februari 25
    1800 Chelsea v Swansea City
    1800 Crystal Palace v Middlesbrough
    1800 Everton v Sunderland
    1800 Hull City v Burnley
    Southampton v Arsenal [IMEAHIRISHWA]
    1800 West Bromwich Albion v Bournemouth
    2030 Watford v West Ham United
    Jumapili Februari 26
    1630 Tottenham Hotspur v Stoke City
    Manchester City v Manchester United[IMEAHIRISHWA]
    Jumatatu Februari 27
    2300 Leicester City v Liverpool
    Jumamosi Machi 4
    1530 Manchester United v Bournemouth
    1800 Leicester City v Hull City
    1800 Stoke City v Middlesbrough
    1800 Swansea City v Burnley
    1800 Watford v Southampton
    1800 West Bromwich Albion v Crystal Palace
    2030 Liverpool v Arsenal
    Jumapili Machi 5
    1630 Tottenham Hotspur v Everton
    1900 Sunderland v Manchester City
    Jumatatu Machi 6
    2300 West Ham United v Chelsea

    FULL TIME: BURNLEY 1 v 1 CHELSEA, BLUES WADUWAA SARE, BRADY NDIYE ALIYESAWAZISHA BAO!

    By: Unknown On: Jumatatu, Februari 13, 2017
  • Share The Gag

  • Chelsea Leo wameikosa nafasi ya kwenda Pointi 12 mbele baada ya kutoka Sare na Burnley huko Turf Moor.
    Chelsea sasa wako Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Tottenham lakini Jumatatu Usiku Manchester City wanaweza kutwaa Nafasi ya Pili na pengo lao na Chelsea kuwa Pointi 8 ikiwa wataifunga Bournemouth Ugenini.

    Hii Leo Chelsea walitangulia kufunga Dakika ya 7 kwa Bao la Pedro lakini Robbie Brady akaisawazishia Burnley Dakika ya 24 kwa Frikiki kali.

    Matokeo haya yanawaweka Burnley Nafasi ya 12 na kudumisha rekodi yao ya kuwa wagumu mno wakiwa kwao Turf Moor.

    Jumapili, 5 Februari 2017

    Baada ya uteja wa fainali mbili za AFCON, Cameroon imelipa kisasi kwa Misri

    By: Unknown On: Jumapili, Februari 05, 2017
  • Share The Gag


  • Usiku wa February 5 ndio siku ambayo mchezo wa fainali ya mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON 2017 ulichezwa,  mchezo wa fainali ya AFCON 2017 ulikuwa unazikutanisha timu za Misri dhidi ya Cameroon, lakini Cameroon wamefanikiwa kufuta uteja kwa kufungwa fainali mbili na Misri.

    Cameroon wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1, Nicolas N’koulou alifunga goli la kusawazishia Cameroon dakika ya 58 baada ya Mohamed Elneny kuifungia Misri goli la uongozi dakika ya 22, Vincent Aboubakar ndio alizima ndoto za Misri baada ya dakika ya 88 kufunga goli la ushindi.

    Ushindi huo unakuja baada ya Cameroon kufumgwa fainali mbili za AFCON na Misri, alifungwa fainali ya AFCON 2008 goli 1-0 Mohamed Aboutrika akifunga goli hilo, lakini walipoteza fainali ya AFCON 1986, Cameroon wanakuwa wamechukua taji lao la tano la AFCON wakati Misri wanabakia na rekodi yao ya kuchukua mataji nane ya AFCON.

    Rekodi nyingine zilizowekwa katika AFCON na Cameroon ni kuwa inakuwa timu ya kwanza kuwahi kuifunga Misri goli katika fainali za AFCON baada ya Ethiopia, huku kocha wa Misri Hector Raul  Cuper akiendeleza rekodi yake mbovu kwa kupoteza fainali yake ya sita katika soka akiwa kama kocha wa timu tofauti.

    LEICESTER CITY 0 vs 3 MANCHESTER UNITED

    By: Unknown On: Jumapili, Februari 05, 2017
  • Share The Gag

  • Ibra akishangilia bao lake MANCHESTER UNITED imewatandika Mabingwa wa England Leicester City 3-0 wakiwa kwao King Power Stadium kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
    Ushindi huu umewabakiza Man United Nafasi ya 6 lakini sasa wapo Pointi 1 nyuma ya Timu ya 5 Liverpool, Pointi 2 nyuma ya Timu ya 4 Arsenal, Pointi 4 nyuma ya Timu ya 3 Man City na Pointi 5 nyuma ya Timu ya Pili Spurs huku Chelsea wakiwa kileleni Pointi 14 mbele ya Man United.

    Man United walipata Bao lao la kwanza Dakika ya 41 baada ya Kichwa cha Chris Smalling kuwahiwa na Mkhitaryan kabla Beki wa Leicester Huth kuukuta Mpira na kumtoka Beki mwingine wa Leicester Morgan na kumchambua Kipa Schmeichel.

    Sekunde 87 baada ya Bao hilo Man United walikuwa 2-0 mbele kwa Bao la Zlatan Ibrahimovic alieunganisha Krosi ya Valencia.
    Hadi Mapumziko Leicester 0 Man United 2.

    Kipindi cha Pili kuanza Timu zote zilifanya mabadiliko kwa Leicester kuwaingiza King na Gray kuwabadili Musa na Okazakina huku Man United wakimtoa Marcos Rojo na kumwingiza Daley Blind.
    Man United walifunga Bao la 3 Dakika ya 49 kufuatia ushirikiano mwema wa Ibrahimovic na Mkhitaryan kumfungulia Juan Mata kupiga Bao.

    AFCON 2017: EGYPT 1 vs 2 CAMEROON, NICOLAS NA VINCENT WAIONGOZA CAMEROON KULIPA KISASI NA KUTWAA KOMBE!

    By: Unknown On: Jumapili, Februari 05, 2017
  • Share The Gag


  • http://a1.espncdn.com/combiner/i?img=%2Fphoto%2F2017%2F0205%2Fr178232_1296x518_5%2D2.jpg&w=1006&h=402&scale=crop&cquality=80&location=originBao la Egypt lilifungwa na Mohamed Elneny dakika ya (22')

    Huku Nicolas N'Koulou akiisawazishia bao dakika ya (59') kipindi cha pili na dakika za lala salama Vincent Aboubakar aliipa bao dakika ya (88') na mtanange kumalizika kwa 2-1.


    Ijumaa, 3 Februari 2017

    MSIMAMO WA LIGI KUU ENGLAND ULIVYO KWA SASA: CHELSEA BADO KILELENI,SPURS NA ARSENAL WANAFUATA!

    By: Unknown On: Ijumaa, Februari 03, 2017
  • Share The Gag

  • MSIMAMO WA LIGI KUU ENGLAND ULIVYO KWA SASA:
    PosLogo &TeamPWDLGDPts
    1ChelseaChelsea2318233256
    2Tottenham HotspurTottenham Hotspur2313822947
    3ArsenalArsenal2314542647
    4LiverpoolLiverpool2313732446
    5Manchester CityManchester City2314451946
    6Manchester UnitedManchester United2311931242
    7EvertonEverton2310761037
    8West Bromwich AlbionWest Bromwich Albion23968233
    9Stoke CityStoke City23788-629
    10BurnleyBurnley239212-829
    11West Ham UnitedWest Ham United238411-1128
    12SouthamptonSouthampton237610-527
    13WatfordWatford237610-1227
    14BournemouthBournemouth237511-926
    15MiddlesbroughMiddlesbrough234910-721
    16Leicester CityLeicester City235612-1421
    17Swansea CitySwansea City236314-2421
    18Crystal PalaceCrystal Palace235414-919
    19Hull CityHull City234514-2717
    20SunderlandSunderland234415-2216

    AFCON 2017: EGYPT YASONGA FAINALI KWA MATUTA (3-4), LEO GHANA AU CAMEROON NANI KUMVAA EGYPT FAINALI?

    By: Unknown On: Ijumaa, Februari 03, 2017
  • Share The Gag

  • EGYPT wametinga Fainali ya AFCON 2017, Kombe la Mataifa ya Afrika, nah ii ni mara yao ya 9 kufanya hilo na kuikuta Rekodi ya kucheza Fainali nyingi baada ya Jana huko
    Stade de I'Amitie, Libreville Nchini Gabon kuibwaga Burkina Faso 4-3 kwa Mikwaju ya Penati Tano Tano kufuatia Sare ya 1-1 katika Dakika 120.
    Kipa Vterani wa Egypt, Essam El Hadary, mwenye Miaka 44, ndie alikuwa Shujaa kwa kuokoa Penati ya Bertrand Traore na kuwapa Egypt ushindi.

    Katika Mechi hiyo, Egypt walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 65 la Mohamed Salah na Burkina Faso kusawazisha Dakika ya 72 kupitia Aristide Bance.
    Kwenye Fainali, Egypt watapambana na Mshindi kati ya Ghana na Cameroon wanaopambana Leo huko Libreville, Gabon.
    VIKOSI:
    BURKINA FASO:
    Koffi, Yago, Dayo, B. Koné, Y. Coulibaly, Kaboré, I. Touré, R. Traoré (Diawara 80'), B. Traoré, Bancé (A.Traore 102'), Nakoulma.

    EGYPT:
    El-Hadary, El Mohamady (Gaber 106'), Hegazy, Gabr, Fathy, Hamed, M. Salah, I. Salah, Said, Trezeguet (Sobhi 85'), Kahraba (Warda 76')

    AFCON 2017

    RATIBA
    Robo Fainali
    Jumamosi Januari 28

    Burkina Faso 2 Tunisia 0 [RF 1]
    Senegal 0 Cameroon 0 [Penati 4-5] [RF 2]

    Jumapili Januari 29

    Congo DR 1 Ghana 2 [RF 3]
    Egypt 1 Morocco 0 [RF 4]
    Nusu Fainali
    Jumatano Februari 1
    Burkina Faso 1 Egypt 1
    Alhamisi Februari 2
    2200 Cameroon v Ghana
    Mshindi wa 3
    Jumamosi Februari 4
    2200 Burkina Faso v Aliefungwa NF 2
    Fainali
    Jumapili Februari 5

    2200 Egypt v Mshindi NF 2

    NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA:
    -Egypt-Mara 7
    -Cameroon, Ghana-Mara 4
    -Nigeria-Mara 3
    -Congo DR-Mara 2
    -Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1

    COPA DEL REY, NUSU FAINALI: SUAREZ, MESSI WAIZAMISHA ATLETICO KWAO VICENTE CALDERON BAO 2-1.

    By: Unknown On: Ijumaa, Februari 03, 2017
  • Share The Gag

  • 2-1Stefan Savic is proving a problem at the back for Atletico MadridMabingwa Watetezi wa Kombe la Mfalme wa Spain, Copa del Rey, Barcelona usiku  wameichapa Atletico Madrid Bao 2-1 huko Estadio Vicente Calderon Jijini Madrid katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali.
    Timu hizi zitarudiana Wiki ijayo huko Nou Camp na Mshindi kucheza na Mshindi wa Nusu Fainali nyingine kati ya Deportivo Alaves na Celta Vigo ambao Leo wanacheza Mechi yao ya Kwanza.

    Atletico forward Antoine Griezmannheads to score a goalKwenye Mechi ya Jana, Luis Suarez ndie aliifungia Barca Bao la Kwanza katika Dakika ya 7 alipokokota Mpira toka Mstari wa Kati na kufunga kilaini.
    Barcelona's Lionel Messi celebrates a goal with Luis Suarez
    Dakika ya 33 mzinga wa Lionel Messi kutoka nje ya Boksi uligonga Posti na kutinga na kuwapa Barca Bao la Pili.
    Dakika ya 59, Antoine Griezmann akaipa matumaini Atletico baada ya kufunga Bao pekee kwao.
    Barcelona's Luis Suarez scores their first goalLA LIGA
    Copa del Rey – Nusu Fainali
    Jumatano Februari 1

    Atletico Madrid 1 Barcelona 1

    Alhamisi Februari 2

    2300 Celta Vigo v Deportivo Alaves

    Mechi za Pili
    [Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
    Jumanne Februari 7

    2300 Barcelona v Atletico Madrid [2-1]

    Jumatano Februari 8
    2300 Deportivo Alaves v Celta Vigo

    EPL: MAN CITY YAISHUSHIA KIPIGO KIZITO WEST HAM, MAN UNITED YABANWA MBAVU, STOKE CITY NA EVERTON NAO WALALA KWA SARE!

    By: Unknown On: Ijumaa, Februari 03, 2017
  • Share The Gag

  • Ligi Kuu England imeendelea Jana kwa Mechi 3 na Manchester City kuibuka washindi wakubwa kwa kuicharaza West Ham 4-0 wakati Manchester United ikitoka 0-0 na Hull City na Stoke City na Everton kutoka 1-1.
    Huko London Stadium Jijini London, Wenyeji West Ham walibandikwa Bao 4-0 na Man City kwa Bao za Kevin De Bruyne, David Silva, Gabriel Jesus na Yaya Toure.
    Matokeo hayo yamewabakisha City Nafasi ya 5.
    Huko Old Trafford, Kipa wa Hull City Eldin Jakupovic aliikosesha ushindi Man United kwa kuokoa Bao za wazi kadhaa na hasa michomo ya Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba.
    Matokeo hayo yamewabakisha Man United Nafasi ya 5 ingawa hawajafungwa katika Mechi zao 14 zilizopita za Ligi lakini Sare hii ya 3 mfululizo ndio inawatafuna na kuwabakisha Nafasi hiyo ya 6 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya 5 City na Liverpool zinazofungana kwa Pointi.

    Huko Britannia Stadium, Wenyeji Stoke City na Everton zilitoka Sare 1-1 na Wafungaji walikuwa Peter Crouch kwa Stoke na Ryan Shawcross aliejifunga mwenyewe kuisawazishia Everton.

    Kwa Crouch, hilo lilikuwa Bao lake la 100 la Ligi. 


    EPL – Ligi Kuu England

    RATIBA
    Jumamosi Februari 4

    1530 Chelsea v Arsenal
    1800 Crystal Palace v Sunderland
    1800 Everton v Bournemouth
    1800 Hull City v Liverpool
    1800 Southampton v West Ham United
    1800 Watford v Burnley
    1800 West Bromwich Albion v Stoke City
    2030 Tottenham Hotspur v Middlesbrough

    Jumapili Februari 5

    1630 Manchester City v Swansea City

    1900 Leicester City v Manchester United

    EMMANUEL ADEBAYOR AZIPIGA CHINI TIMU ZA ENGLAND, AJIUNGA NA TIMU YA INSTANBUL BASAKSEHIR

    By: Unknown On: Ijumaa, Februari 03, 2017
  • Share The Gag


  • Emmanuel Adebayor amejiunga na Timu ya Istanbul Basaksehir