.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumamosi, 14 Machi 2015

Tagged Under:

BASI LAGONGA MKOKOTENI WA NG'OMBE HUKO SIMIYU, LAUA , 34 WANUSURIKA KUFA

By: Unknown On: Jumamosi, Machi 14, 2015
  • Share The Gag
  •  
    Basi la Simiyu Express linalofanya safari zake Dar - Simiyu kila siku limepata ajali kwa kugonga mkokoteni unaosukumwa na ng'ombe na kuua mtu mmoja na ng'ombe wote leo saa sita mchana
    mkoani Simiyu katika kijiji cha Salunda barabara kuu iendayo Shinyanga.
    Hakuna abiria aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa ila kiongozi wa mkokoteni.dereva alifariki dunia na ng'ombe wake wawili walifariki pia.

    Basi aina ya Scania lenye namba za asajili  T396 AMP Kampuni ya Simiyu Express mali ya Adinan Khan Mkazi wa Dar es salaam linalofanya safari zake Mkoani Simiyu-Dar es salaam, likiwa kwenye kichaka baada ya kupata ajali muda mfupi baada ya kutoka stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

    Inaelezwa kuwa baada ya kuacha njia likiwa katika mwendo kasi lilikutana na mkokota toroli la ngo'mbe akiwa katikati ya barabra maeneo ya Salunda kata ya Bariadi Mjini .

    Kufuatia hali hiyo basi hilo lilimgonga mkokota toroli aitwaye Bahati Suti (25) Mkazi wa Musoma wilayani Itilima Mkoani Simiyu ambaye alifariki dunia  papo hapo , huku ngo'mbe 2 na wakipoteza uhai papo hapo.

     Kamanda wa polisi Mkoani Simiyu  Charles Mkumbo amesema basi hilo lilikuwa likiendeshwa na Ramadhan Hassan (30) mkazi wa Magomeni Kagera Jijini Dar es salaam, na kwamba kufuatia ajali hiyo gari hilo liliharibika kioo cha mbele pamoja na bampa na dereva wa basi  anashikiliwa na jeshi la polisi.
     Abiria wote 34 katika basi hilo ni wazima.

    Baadhi ya wasamaria wema wakikokota mkokoteni uliosababisha ajali hiyo na kupoteza uhai wa dereva wake pamoja na Ngo'mbe 2.

    Baadhi ya mashuhuda wakiangalia basi hilo

    Mashuhuda.

    Ngo'mbe akiwa amekufa


    Baada ya basi kutolewa kichakani, muonekano wake lilivyopata ajali





    0 maoni:

    Chapisha Maoni