Ushindi huu wa Blatter umekuja baada ya kugubikwa na Kashfa ya Rushwa iliyotokana na hatua ya Marekani kufungua Mashitaka kwa Maafisa wa FIFA kwa tuhuma za rushwa Siku moja tu kabla Uchaguzi huo kufanyika.
Ingawa katika Raundi ya Kwanza ya Kura si Blatter wala Mpinzani wake Prince Ali bin Al Hussein alieshinda Theluthi mbili ya Kura ili kushinda Uchaguzi huo wa Uraisi baada ya Blatter kupata Kura 133 na Prince Ali kupata 73, kitu ambacho kingepeleka Kura kupigwa tena, Mjordan huyo aliamua kubwaga manyanga na kukubali kushindwa.
Akipokea
ushindi wake kwa vifijo Ukumbini, Blatter alitamba: "Twende FIFA,
Twende FIFA!" Mapema hii Leo, akiongea kwenye Mkutano wa Kongresi ya
FIFA, Blatter alisema kama Uenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Miaka
ya 2018 na 2022 ungeenda kwa Nchi nyingine na si Russia na Qatar basi
kashfa hiyo ya Rushwa isingekuwepo.
0 maoni:
Chapisha Maoni