.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 31 Desemba 2015

MSANII TEKNO MILES KUNOGESHA TAMASHA LA JOHNNIE WALKER “GROWN & SEXY THE GOLD FINALE”

By: Unknown On: Alhamisi, Desemba 31, 2015
  • Share The Gag

  •  Msanii Tekno Miles (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla iliyomtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Msanii huyo anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya ambapo pia atafunga rasmi mfululizo wa matamasha hayo ya Grown And Sexy tokea kuanzishwa kwake.
    Dj rasmi wa msanii Jay Z wa Marekani al maarufu kama “Young Guru” akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ya kumtambulisha rasmi Msanii Tekno Miles (Katikati) ambaye anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya. Dj huyo atasimamia vilivyo kazi yake katika shughuli nzima ya Tamasha hilo. 
    Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija (Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Msanii Tekno Miles (wa kwanza kushoto) na Dj rasmi wa msanii Jay Z wa Marekani al maarufu kama “Young Guru” wakati wa hafla iliyomtambulisha Msanii Tekno Miles kwa waandishi wa habari iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Msanii huyo anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya ambapo pia atafunga rasmi mfululizo wa matamasha hayo ya Grown And Sexy tokea kuanzishwa kwake. 


    Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa umakini mkutano wa kumtambulisha Msanii maarufu Tekno Miles kutoka Nigeria uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ambaye anatarajiwa kutumbuiza katika mkesha wa Tamasha la Grown and Sexy the Gold finale litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite jijini Dar es salaam.



    Maandalizi ya Tamasha maarufu la Johnnie Walker “Grown and Sexy The Gold finale” kwa ajili ya kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya yanaendelea vizuri ambapo kwa mujibu wa waandaaji wa Tamasha hilo, “Capital events” kupitia wadhamini wao “Johnnie Walker” chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti wamemleta Msanii Tekno Miles kutoka Nigeria kutumbuiza laivu katika Tamasha hilo ambalo litakua la mwisho kabisa katika historia ya matamasha ya Grown and Sexy nchini Tanzania.

    Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam,Meneja chapa wa pombe kali SBL Shomari Shija alisema, “Tumeamua kulidhamini Tamasha hili kama njia mojawapo ya kujumuika na kufurahi kwa pamoja na wateja wetu wa chapa za Johnnie Walker katika kuuaga rasmi mwaka huu wa 2015.
    Bw. Shija aliongeza kuwa katika Tamasha la mwaka huu ambalo ni la mwisho katika historia ya mfululizo wa matamasha ya Grown and Sexy waliona ni vema kumleta msanii maarufu toka Nigeria “Tekno Miles” ambaye aliwasili jana usiku mida ya saa nane akitokea Nigeria tayari kwa kulipamba Tamasha hilo. Msanii huyo ambaye anatamba na vibao mbalimbali kwenye anga ya muziki hivi sasa kama Shoki, Duro na Wash atatumbuiza laivu kwenye Tamasha hilo ambalo litafanyika siku ya mkesha wa mwaka mpya katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga, Msasani karibu na Best Bite.
    Sambamba na uwepo wa msanii huyo wengine wataopamba Tamasha hilo ni Dj Maarufu “Young Guru” ambaye ni Dj rasmi wa msanii Jay Z toka Marekani ambaye ataisimamia shoo hiyo vilivyo pamoja na malkia wa uswazi mwanadada “Shaa” kisura wa Tamasha hilo ambaye atasherehesha shughuli nzima katika usiku wa tukio.
    Kwa upande wake Msanii Tekno alisema anafurahia kusherekea mkesha wa mwaka mpya akiwa Tanzania na kuahidi kuporomosha burudani ya nguvu kwa mashabiki wake watakaojitokeza kushuhudia Tamasha hilo la kufunga mwaka.



    Naye Mwakilishi wa Capital events waandaaji wa Tamasha hilo Bw. Justin Massawe alisema “Tunawakaribisha wapenzi wote wa burudani na chapa ya Johnnie Walker kujitokeza kwa wingi kushuhudia Tamasha letu la mwisho la Grown & Sexy na kuahidi kuwa litakuwa la kufana zaidi kwani wamejipanga kutoa burudani ya nguvu na kuwafurahisha mashabiki mbalimbali.

    “Ningependa kuwashukuru wadhamini wetu mbalimbali katika kipindi chote cha mfululizo wa matamasha haya tokea yalipoanzishwa rasmi kwa ushirikiano mzuri ambao wametupatia hadi hii leo tunapofunga rasmi tamasha hili la mwisho la Grown and Sexy the Gold finale.”
    Bw. Justin hakusita pia kuwashukuru Johnnie Walker kwa kuhakikisha wanakamilisha mikataba yote ya kumleta msanii Tekno Miles pamoja na Dj Young Guru hapa nchini na kwa kuhakikisha kwamba tamasha la mwisho linakamilika kwa mafanikio” makubwa zaidi.

    FT..SUNDERLAND 0 v 1 LIVERPOOL, BENTEKE AIPA USHINDI LIVERPOOL...NA KUIPUMULIA MAN UNITED!

    By: Unknown On: Alhamisi, Desemba 31, 2015
  • Share The Gag

  • Benteke tayari ameishaipatia bao la kuongoza Liverpool kwa 1-0

    BAO pekee la Christian Benteke limewapa Liverpool ushindi wa Bao 1-0 walipocheza huko Stadium of Light na Sunderland katika Mechi ya mwisho kabisa ya Ligi Kuu England.
    Bao hilo lilipatikana Dakika 1 tu baada ya Kipindi cha Pili kuanza kwa Nathanial Clyne kupenyeza Mpira mbele na Adam Lallana kuugusa tu na kumkuta Christian Benteke aliefunga na kuipa Bao Liverpool.
    Ushindi huu umewaweka Liverpool Nafasi ya 7 wakiwa Pointi sawa na Man United waliowazidi kwa ubora wa magoli.
    Raha tupu!Reta akiutazama mpira kama upo ndani ya eneo la Kona kisawasawa!

    DAVID MOYES AIOMBA KLABU YA MAN UNITED IMPATIE MUDA MENEJA LOUIS VAN GAAL

    By: Unknown On: Alhamisi, Desemba 31, 2015
  • Share The Gag

  • www.bukobasports.comMENEJA wa zamani wa Manchester United David Moyes ameihimiza Klabu hiyo kumpa muda zaidi Meneja wa sasa Louis van Gaal.
    Hivi sasa Van Gaal yupo kwenye presha kubwa baada ya Man United kutoshinda katika Mechi zao 8 zilizopita na kufungwa Mechi 3 mfululizo za Ligi Kuu England na kuporomoka hadi Nafasi ya 6 kwenye Ligi Kuu England.
    Lakini David Moyes, ambae alidumu Miezi 10 tu Man United baada ya kumrithi Sir Alex Ferguson aliekaa kwa Miaka 26, anaona Man United itaweka misingi mibovu ikiwa pia itamfukuza Van Gaal muda mfupi tu kama yeye.
    Van Gaal sasa yupo Man United kwa Miezi 18.
    Akiongea kwenye Kipindi cha BT Sport 1, Moyes alisema: “Nadhani msimamo wa Manchester United ni kubaki na Mameneja wao, Siku zote wanawasapoti Mameneja wao.”
    “Natumai watabaki nae Van Gaal, anajenga Timu mpya na hilo huchukua muda. Sidhani kama wanataka kuwa Klabu inayobadili Mameneja kila kukicha.”
    Sir Alex Ferguson alitwaa Makombe 38 akiwa na Man United na alipostaafu tu Msimu uliofuatia, Moyes alichukua wadhifa na Man United kumaliza ya 7 kwenye Ligi na kukosa kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI.
    Lakini katika Msimu wake wa kwanza tu na Man United, Van Gaal aliiwezesha Timu kumaliza ndani ya 4 Bora na kurejea kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI.
    Hata hivyo, David Moyes amesema ni wazi kumrithi Sir Alex Ferguson ni kitu kigumu na pia kuondoka kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu, David Gill, wakati huo huo kama Ferguson kumeathiri Klabu.
    akini Moyes bado analalamika kutimuliwa Man United baada ya muda mfupi kwani aliamini yuko hapo na atabaki hapo kwa muda mrefu ili kuijenga upya Timu baada ya Sir Alex Ferguson.­

    RONALDO BADO NI BALAA AIPA USHINDI REAL LEO!

    By: Unknown On: Alhamisi, Desemba 31, 2015
  • Share The Gag

  • Ronaldo akishangilia moja ya  bao lakeLeo La Liga imerejea tena na ndani ya Santiago Bernabeu, Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo aliiongoza Real Madrid kuichapa Real Sociedad Bao 3-1 na kuongoza Ligi hii ya Spain pengine kwa muda tu hadi baadae Usiku huu.
    Ronaldo alikosa kuipa Real Bao wakati walipopewa Penati na yeye kuipaisha juu lakini Dakika ya 42 wakapata Penati nyingine na yeye kupiga tena na kufunga.
    Hadi Mapumziko, Real 1 Sociedad 0.
    Dakika 4 tu baada ya Kipindi cha Pili kuanza Real Sociedad wakasawazisha kwa Bao la Armindo Bruma lakini Ronaldo akaipa Real Bao la Pili alipounganisha Kona ya Marcelo.

    Bao la 3 kwa Real lilifungwa na Lucas Vazquez, alieingizwa Kipindi cha Pili kumbadili Karim Benzema, na hilo kuwa Bao lake la kwanza kabisa kwa Real.

    Jumatano, 30 Desemba 2015

    RATIBA: LA LIGA UWANJANI LEO MECHI ZA FUNGA MWAKA 2015, REAL MDRID v REAL SOCIEDAD, BARCELONA v REAL BETIS

    By: Unknown On: Jumatano, Desemba 30, 2015
  • Share The Gag

  • www.bukobasports.comLA LIGA
    RATIBA
    Jumatano Desemba 30

    18:00 Real Madrid CF v Real Sociedad
    18:00 Levante v Malaga CF
    20:15 Rayo Vallecano v Atletico de Madrid
    20:15 Sevilla FC v RCD Espanyol
    20:30 SD Eibar v Sporting Gijon
    22:30 FC Barcelona v Real Betis
    22:30 Celta de Vigo v Athletic de Bilbao
    22:30 Getafe CF v Deportivo La Coruna
    23:00 Las Palmas v Granada CF
    Alhamisi Desemba 31
    18:00 Villarreal CF v Valencia C.F

    MSIMAMO ULIVYO KWA SASA:

    By: Unknown On: Jumatano, Desemba 30, 2015
  • Share The Gag


  • Barclays Premier League
    PosLogo &TeamPWDLGDPts
    1ArsenalArsenal1912341539
    2Leicester CityLeicester City1911621239
    3Manchester CityManchester City1911351736
    4Tottenham HotspurTottenham Hotspur199821835
    5Crystal PalaceCrystal Palace19946731
    6Manchester UnitedManchester United19865630
    7West Ham UnitedWest Ham United19784529
    8WatfordWatford19856429
    9Stoke CityStoke City19856129
    10LiverpoolLiverpool18765-127
    11EvertonEverton19685726
    12SouthamptonSouthampton19667324
    13West Bromwich AlbionWest Bromwich Albion19658-623
    14ChelseaChelsea19559-620
    15Norwich CityNorwich City19559-1020
    16BournemouthBournemouth19559-1220
    17Swansea CitySwansea City19478-819
    18Newcastle UnitedNewcastle United194510-1517
    19SunderlandSunderland183312-1812
    20Aston VillaAston Villa191513-198

    KIWANGO SAFI CHA MAN UNITED KWA KUTOKA SARE YA 0-0 NA CHELSEA, BODI YA MAN UNITED YAKUBALIANA NA VAN GAAL KUENDELEA NAE!

    By: Unknown On: Jumatano, Desemba 30, 2015
  • Share The Gag

  • MARA baada ya Jumatatu Usiku kutoka Sare 0-0 na Mabingwa Watetezi Chelsea Uwanjani Old Trafford na kusitisha wimbi la kufungwa Mechi 4 mfululizo, Meneja wa Manchester United Louis van Gaal aliibuka na kutamba hana mipango ya kujiuzulu.
    Baada ya kuchapwa 2-0 na Stoke City Siku ya Boksing Dei, Man United waliibuka na kusakata Soka safi na kustahili kuifunga Chelsea lakini, kama kawaida, umaliziaji uliwaangusha.
    Hali hiyo ilimfanya Louis van Gaal apige ‘abauti tani’ na kudai Wachezaji wake wamempa sababu ya kutojiuzulu tofauti na alivyodokeza huko Britannia Stadium mara baada ya kufungwa na Stoke. Jana Van Gaal alisema: “Wachezaji wakicheza namna ile hasa wakati huu wa presha kubwa, hamna sababu ya mimi kujiuzulu. Labda Vyombo vya Habari wanataka hivyo, ila sitafanya.”
    Wakati huo huo, Mchambuzi wa Soka anaeaminika huko England, Andy Gray, Mchezaji wa zamani wa Scotland aliechezea Klabu kadhaa huko England, amedai Man United hawana uchu wa kumwajiri Jose Mourinho kama Meneja.
    Mourinho, ambae alitimuliwa na Chelsea Wiki iliyokwisha, amekuwa akitajwa na wengi kuwa atachukua wadhifa wa Van Gaal.

    Jumatatu, nje ya Old Trafford, kwenye Mechi na Chelsea, Wachuuzi walikuwa wakitembeza bidhaa kadhaa zikiwa na Nembo ya Man United na Jina la Jose Mourinho wakimpigia debe kuwa Meneja wa Man United.
    Lakini Andy Gray anaamini Bodi ya Man United bado inamsapoti Van Gaal na haimtaki Mourinho ambae wanaona hulka yake haiendani na utamaduni wa Man United.

    LEO NDANI YA KING POWER STADIUM: LEICESTER vs MANCHESTER CITY, NANI KUIBUKA KIDEDEA?

    By: Unknown On: Jumatano, Desemba 30, 2015
  • Share The Gag

  • Patashika za Ligi Kuu England kuendelea tena leo, Kuna Mechi moja pekee ambayo itaamua nani anamaliza 2015 akiwa anaongoza Ligi.
    Jana, Arsenal iliichapa Bournemouth 2-0 na kutwaa uongozi wa Ligi wakiwa na Pointi 39 kwa Mechi 19 wakifuata Leicester wenye Pointi 38 kwa Mechi 18, Tottenham ni wa 3 na wana Pointi 35 kwa Mechi 19 na wa 4 ni Man City wenye Pointi 35 kwa Mechi 18.
    Leo huko King Power Stadium, Leicester wanacheza na Man City na wakishinda watarudi kileleni na wakitoka Sare watabaki Nafasi ya Pili.
    Ikiwa City itashinda basi watapanda hadi Nafasi ya Pili.
    Leicester wanatinga kwenye Mechi hii wakitoka kufungwa 1-0 na Liverpool na kupoteza wimbi lao la kutofungwa katika Mechi 10 wakati City ikiichapa Sunderland 4-1.
    Wakati Leicester wana Kikosi kamili bila Majeruhi ingawa mapema walipatwa na wasiwasi wa Staa wao Jamie Vardy, ambae ndie Mfungaji Bora wa Ligi, kutocheza kutokana na kuugua, City watamkosa Nahodha wao Vincent Kompany ambae ni Majeruhi pamoja na majeruhi wengine Pablo Zabaleta, Fernando na Samir Nasri.
    Yaya Toure kendeleza tena wimbi la magoli!

    TOP 20 ya wachezaji bora wa Ligi Kuu Uingereza 2015, Afrika imetoa wachezaji wawili pekee, Cheki list hapa …

    By: Unknown On: Jumatano, Desemba 30, 2015
  • Share The Gag

  • Tukiwa tunaelekea kuumaliza mwaka 2015 na kuingia mwaka mpya 2016 moja kati ya mitandao inayoandika stori za michezo duniani imeandika TOP ya wachezaji bora wakali wa Ligi Kuu Uingereza. Mtandao wa bleacherreport.com umeandika list ya wachezaji 20 wakali wa Ligi Kuu Uingereza kwa mwaka 2015.
    Hii ndio list ya majina yote 20 mtu wangu.
    1. David De Gea (Man United/Hispania)
    2. Mesut Ozil (Arsenal/Ujerumani)
    3. Alexis Sanchez ( Arsenal/Chile)
    4. David Silva (Man City/Hispania)
    5. Sergio Aguero (Man City/Argentina)
    6. Chris Smalling (Man United/Uingereza)
    7. Santi Cazorla (Arsenal/Hispania)
    8. Harry Kane (Tottenham/Uingereza)
    9. Toby Alderweireld (Tottenham/Ubelgiji)
    10. Francis Coquelin (Arsenal/Ufaransa)
    11. Willian (Chelsea/Brazil)
    12. Riyad Mahrez (Leicester City/Algeria)
    13. Jamie Vardy (Leicester City/Uingereza)
    14. Philippe Coutinho (Liverpool/Brazil)
    15. Hector Bellerin (Arsenal/Hispania)
    16. Hugo Lloris (Tottenham/Ufaransa)
    17. Morgan Schneiderlin (Man United/Ufaransa)
    18. Scott Dann (Crystal Palace/ Uingereza)
    19. Sadio Mane (Southampton/Senegal)
    20. John Stones (Everton/Uingereza)

    Jumatatu, 28 Desemba 2015

    WAZIRI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII PROF. JUMANNE MAGHEMBE AWASILI MAKAO MAKUU YA WIZARA HIYO MPINGO HOUSE MARA BAADA YA KUAPISHWA IKULU LEO

    By: Unknown On: Jumatatu, Desemba 28, 2015
  • Share The Gag
  •  
    Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (mbele kulia) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Selestine Gesimba wakati wa mapokezi yake leo tarehe 28 Desemba 2015 katika ofisi yake mpya Mpingo House mara baada ya kuapishwa Ikulu mapema asubuhi ya leo. Nyuma yake kulia ni naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Ramo Makani na anaeongoza utambulisho katikati yao ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru.
     Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akisaini kitabu cha wageni mara tu baada ya kuingia katika ofisi yake mpya iliyopo Mpingo House mapema leo tarehe 28 Desemba 2015 baada ya kuapishwa Ikulu na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Wanaoshuhudia kulia ni Naibu Wazari wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Ramo Makani na Katibu Mkuu Dkt. Adelhelm Meru (kushoto).
    Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (kushoto) na Naibu Waziri Mhe. Eng. Ramo Makani (kulia) mara baada ya kusaini kitabu cha wageni ofisini kwake mapema leo tarehe 28 Desemba 2015.
    Picha ya pamoja kati ya Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) na Naibu Waziri wake Mhe. Eng. Ramo Makani (wa pili kushoto), Katibu Mkuu wa Wziara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (wa kwanza kulia) na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Selestine Gesimba(kushoto). 
    Sehemu ya wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa tayari kwa mapokezi ya Waziri wao mpya Mhe. Prof. Jumanne Maghembe aliyeapishwa Ikulu leo na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania Mhe. John Pombe Magufuli.(Picha na Hamza Temba - Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii)