
Kombe hilo, ambalo lilianza Mwaka 1871-1872, limekuwa halina Mdhamini tangu Msimu uliopita baada ya Kampuni ya Bia, Budweiser, kumaliza Mkataba na FA, Chama cha Soka England.
FA sasa imeingia Mkataba na Kampuni ya Ndege ya Dubai, Emirates, kuwa Wadhamini wa Kombe hilo kwa Miaka Mitatu hadi 2018.
Habari hizi za udhamini huu zimethibitishwa na Mwenyekiti wa FA, Greg Dyke, ambae amesema Kampuni ya Ndege ya Emirates ina nia njema kwenye Michezo na ni habari njema kwao, Washabiki na Gemu nzima ya Soka.

0 maoni:
Chapisha Maoni