.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumapili, 31 Mei 2015

Tagged Under:

NAPOLI 2 vs 4 LAZIO,

By: Unknown On: Jumapili, Mei 31, 2015
  • Share The Gag

  • Marco Parolo dakika ya 33 kipindi cha kwanza aliifungia bao Lazio.

    Dakika ya majerhi ya kipindi cha kwanza Antonio Candreva alichomoka na kuwakacha mabeki na  kuwaliwafungia bao dakika ya 45 na kufanya 2-0 dhidi ya Napoli inayoongozwa na Rafael Benitez na kwenda mapumziko ikiwa nyuma ya bao mbili.

    Kipindi cha pili dakika ya 55 Gonzalo Higuaín aliifungia bao Napoli na kufanya 2-1 na mtanange kuanza kuchangamka.

    Lazio walicheza pungufu 10 uwanjani baada ya mwenzao kuoneshwa kadi nyekundu  na baadae Napoli dakika ya 64 Gonzalo Higuaín alisawazisha bao tena na kufanya 2-2.

    Nao Napoli dakika 70 mwenzao Faouzi Ghoulam alioneshwa kadi ya pili ya njano na kisha kuondoshwa kwa kadi nyekundu hivyo kucheza kila Timu wakiwa 10. 

    Dakika ya 75 Napoli walipata penati ya kizushi  na ya Utata na Gonzalo Higuaín kuikosa penati hiyo kwa kupaisha sana mpira juu ya lango la Lazio.

    Dakika ya 85 Ogenyi Onazi wa Lazio aliwamaliza Napoli nguvu pale alipowafunga bao kimaajabu na kuwapa  bao la 3 Lazio.
    Zikiwa zimeongezwa dakika 5 Lazio walipata tena bao la nne baada ya kupigwa frii kiki na M. Klose kuumalizia mpira huo nyavuni baada ya beki wao Napoli kupitwa.
    Na mtanange kumalizika kwa Lazio kuwa washindi wa bao 4-2 dhidi ya Napoli inayoongozwa na Rafael Benitez.

    Napoli wamemaliza msimu wakiwa nafasi ya 5 wakiwa na pointi 63 huku Lazio wakiwa nafasi ya tatu wakiwa na pointi 69.

    Rafael Benitez anaagwa na Napoli kwa kichapo cha bao 4-2 kutoka kwa Lazio huku kukiwa na fununu kwa asilimia kubwa kwa Kocha huyo kuhamia Klabu kubwa ya Spain ya Real Madrid kwenda kuwa mkufunzi wao kwa msimu huu unaokuja wa 2015/16.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni