.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatano, 17 Septemba 2014

MAMBO 5 MUHIMU DANNY WELBECK KU ‘SHAINI’ ARSENAL

By: Unknown On: Jumatano, Septemba 17, 2014
  • Share The Gag

  • Na Simon Chimbo
    Moja kati ya habari kubwa sana za usajili wa kiangazi msimu huu nchini Uingereza ni uhamisho wa mshambuliaji mwenye nguvu na mbio Danny Welbeck kutoka Manchester United kwenda Arsenal kwa ada ya paundi 16m. kijana huyu mwenye miaka 23 pamoja na kubezwa na mashabiki wengi lakini ana kitu ambacho kwa macho ya kawaida hakikuonekana pale Old Trafford. Ndio maana sivishangai vilio vya wakongwe wa Manchester United kama Paul Scholes, David Becham na Rio Ferdinand wakionesha kusikitishwa kwao kwa kuondoka kwa kijana huyo aliyekulia mjini Manchester tangu akiwa mdogo.
    Zifuatazo ni sababu zinazoweza kumng’arisha Dany Welbeck Arsenal;
    1.Kutaka kuthibitisha uwezo wake
    Welbeck kama ambavyo mchezaji yeyote angeweza fanya, atajituma uwanjani ili kuonesha Manchester United walimuuza kimakosa huku pia akitaka kuwaondoa shaka mashabiki wa Arsenal kwamba mzee Wenger hakukosea kumsajili.
    2. Uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza
    Kuumia kwa Olivier Giroud kunamfanya Dany awe na upinzani mdogo na mshambuliaji aliye fiti Yaya Sanogo. Tofauti na ilivyokua Manchester United, Wayne Rooney na Robin Van Persie walimpa wakati mgumu Welbeck kupata nafasi kikosi cha kwanza huku usajili wa Radamel Falcao ungemfanya asipate nafasi kabisa.
    3. Viungo wa Arsenal
    Tofauti na Manchester United ambapo hakukua na viungo wenye uwezo wa kucheza na kutengeneza nafasi kwa washambuliaji wao kufunga magoli, lakini uwezo wa viungo wazuri kama Jack Wilshere, Mesut Ozil, Aaron Ramsey, Carzola na wengine, sina shaka Dany atafunga magoli mengi tofauti na alivyokua Old Trafford.
    4. Matarajio hafifu ya mashabiki wa Arsenal kwa kijana huyo
    Presha sio kubwa kwa Welbeck kufanya vizuri kwa washika mitutu hao wa London kutokana na ukweli kwamba mashabiki wengi wa gunners hawana uhakika na uwezo wa mshambuliaji huyo raia wa Uingereza na hivyo Dany anaweza kucheza vizuri kwani mashabiki hawamtarajii makubwa.
    5.Uwezo wa mwalimu Arsene Wenger

    Wengi mtakubaliana na mimi jinsi Arsene Wenger alivyo wabadilisha wachezaji wake wengi kutoka kua wachezaji wa kawaida hadi kuwa wachezaji wa kiwango cha dunia kama Aaron Ramsey na wenzake huku akiwa na uwezo mkubwa wa kuwa saikoloji wachezaji wake.

    KUNA KITU PEP GUARDIOLA AMEWAONYA MANCHESTER UNITED, NI KIPI HICHO?

    By: Unknown On: Jumatano, Septemba 17, 2014
  • Share The Gag

  • Pep Guardiola has warned Manchester United boss Louis van Gaal he cannot afford his top players
    Pep Guardiola amewaonya Man United

    KOCHA wa Bayern Munich, Pep Guardiola amewaonya Manchester United kuwa hawawezi kumudu kuwanunua wachezaji wake bora na amedai hataki kuona nyota wake kama Arjen Robben, Bastian Schweinsteiger na Thomas Muller wanakwenda kucheza ligi kuu England.
    Aliulizwa jana mchana kama aliwahi kumkataliwa Louis van Gaal kusajili wachezaji wake, Guardiola alitikisa kichwa na kusema: Hawana (United) hawakuwa na hela za kutosha"
    The Bayern boss has issued a hands off warning to Manchester United regarding his star players
    Bosi wa Bayern amezua jambo na kuwaonya Manchester United kuhusu wachezaji wake nyota  

    Jumanne, 16 Septemba 2014

    LIGI YA MABINGWA: ARSENAL KIBARUANA NA DORTMUND, REAL MADRID v BASEL

    By: Unknown On: Jumanne, Septemba 16, 2014
  • Share The Gag

  • Aaron Ramsey and Mesut Ozil celebrate the Welshman's goal away at Dortmund last November, in a game the Gunners won 1-0

    EUROPE: Champions League - Group Stage
    11:45 Benfica-Zenit Petersburg


    11:45 Dortmund-Arsenal


    11:45 Galatasaray-Anderlecht


    11:45 Juventus-Malmo FF


    11:45 Liverpool-Ludogorets


    11:45 Monaco-Bayer Leverkusen


    11:45 Olympiakos Piraeus-Atl. Madrid


    11:45 Real Madrid-Basel

    KAGERA SUGAR KUELEKEA TANGA KUPAMBANA NA JKT

    By: Unknown On: Jumanne, Septemba 16, 2014
  • Share The Gag



  • Kikosi cha Timu ya Wakata Miwa Kagera Sugar wameanza leo hii safari kuelekea jijini Tanga kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi wa Ligi kuu soka Tanzania bara katika uwanja wa CCM Mkwakwani dhidi ya wenyeji Mgambo JKT, septemba 20 mwaka huu.
    Kocha msaidizi wa Kagera Sugar, Murage Kabange amesema klabu hiyo ina jumla ya wachezaji 25 na hii leo tayari wapo safari na viongozi watano kwenda kusaka pointi tatu muhimu.
    Kabange aliongeza kuwa wameamua kuanza safari mapema kwasababu kutoka Kagera kwenda Tanga ni mbali sana.
    Viongozi wa Kagera Sugar
    Ubutu wa safu ya ushambuliaji lilikuwa tatizo la kudumu kwa Kagera Sugar lakini kwa sasa limepata marekebisho kwani wamesajili Vijana wa nguvu msimu huu.
    WAKATA miwa wa Kaitaba, `Wanankulukumbi` Kagera Sugar wakijifua kwenye Uwanja wa Kagera Sugar hivi karibuni tayari kwa Ligi kuu Vodacom sep 20 mwaka huu. Kagera Sugar wataanza ufunguzi wa Ligi kuu Vodacom Ugenini na timu ya Mgambo JKT mkwakwani Mjini Tanga wikiendi hii.
    Kocha huyo alisema: “Tuna imani na vijana wetu kuwa wanaweza kutufikisha tunapotaka, japokuwa ligi ya msimu huu inaonekana itakuwa ngumu, lakini tutajitahidi kupigana ili kuweza kushika nafasi za juu”.



    Wachezaji wa Kagera Sugar wakifaya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Kaitaba Hivi karibuni.

    Baadhi ya Viongozi wa Timu ya Kagera Sugar wakiwa Uwanjani Kaitaba wakishuhudia mazoezi ya Vijana wao. Wakijifua kujiandaa na Ligi Kuu Vodacom msimu mpya 2014/15 inayotarajia kuanza hivi Karibuni sep.20 mwaka huu.


    Murage Kabange, kocha msaidizi wa Kagera Sugar (kulia) tayari amebainisha kuwa mapungufu waliyokuwa nayo katika kikosi chao kuwa wameishayafanyia marekebisho na wako tayari kupambana na Mgambo JKT ya Mjini Tanga.
    Kocha Mkuu wa Kagera Sugar (kulia) Bw. Jackson Mayanja akiangalia vijana wake wakati w mazoezi yao kwenye Uwanja wao wa Nyumbani Kaitaba hivi karibuni

    WAREMBO MISS TANZANIA WAJIFUA GYM KUIWEKA MIILI YAO FITI"

    By: Unknown On: Jumanne, Septemba 16, 2014
  • Share The Gag

  • Warembo wanaoshiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2014 leo wameingia siku ya pili ya kambi yao jijini Dar es Salaam na baada ya semina asubuhi na mapumziko ya mchana jioni hii wamefanya mazoezi katika chumba maalum cha mazoezi ‘Gym’, ungana na mpigapicha wa Father Kidevu Blog katika picha mbalimbali za warembo hao katika kambi yao.