Mabingwa wa Italy, Juventus, wakiwa kwao Juventus Arena Jijini Turin Nchini Italy, wameanza vyema Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI walipowafunga Mabingwa Watetezi Real Madrid Bao 2-1.
Juventus
walipata Bao lao la kwanza Dakika ya 8 kutokana na pasi safi ya
Marchisio kumkuta Carlos Tevez ambae Shuti lake lilitemwa na Kipa wa
Real Casillas na kumkuta Alvaro Morata aliekwamisha Mpira wavuni.
Real walisawazisha Dakika ya 27 kwa Bao la Kichwa la Ronaldo kufuatia krosi ya James Rodriguez. Hadi Haftaimu Magoli yalikuwa 1-1.
Kipindi
cha Pili, Juve walifunga Goli la Pili baada ya kuokoa Kona ya Real na
kuanza kaunta ataki kupitia Morata ambae alimpenyezea Tevez alieangushwa
na Carvajal na Refa wa England Martin Atkinson kutoa Penati. Tevez alifunga Penati hiyo na Juve kutangulia 2-1.
Álvaro Morata dakika ya 8 kipindi cha kwanza akipongezwa baada ya kuifungia bao la mapema Juve.
Ronaldo akiwaomba wenzake Real Madrid kuwa makini baada ya kusawazisha bao kipindi cha kwanza
Ronaldo akipongezwa
1-1
Hadi Nyavuni!
Álvaro Morata dakika ya 8 kipindi cha kwanza anaipachikia bao la kwanza Juventus na kufanya 1-0 dhidi ya Real Madrid.
Pongezi
Dakika ya 27 Cristiano Ronaldo aliwasawazishia bao Real Madrid kwa kufanya 1-1 na mtanange kwenda mapumziko kwa sare.
Tevez akisonga na mpira
Ronaldo akiendesha
Baada Juve kwenda 2-1 mbele wakabadilisha Mfumo na kuanza
kutumia 5-3-2 walipomtoa Sturaro na kumwingiza Barzagli ili kuweka
ngoime ya Masentahafu Watatu ili kutetea uongozi wao kwa kujihami zaidi
na kuvizia mashambulizi ya kushtukiza. Timu hizi zitarudiana tena Mei 13 huko Jijini Madrid Uwanjani Santiago Bernabeu.
Meneja wa Real Carlo Ancelotti
Mashabiki wa Real
Mashabiki wa Juve!
0 maoni:
Chapisha Maoni