.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumamosi, 15 Novemba 2014

Tagged Under:

RAIS KIKWETE ATOKA HOSPITALINI BAADA YA KUPATA NAFUU

By: Unknown On: Jumamosi, Novemba 15, 2014
  • Share The Gag

  • unnamed.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  akisindikizwa na Daktari Bingwa
    Edward Schaeffer kutoka
    Hospitali ya Johns Hopkins alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa
    upasuaji wa kuondoa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya

    kupata nafuu.Kulia nia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete. Hali ya Rais
    Kikwete imezidi kuimarika baada ya kutoka wodini na kuwa mapumzikoni
    akiuguza kidonda kilichotokana na upasuaji aliofanyiwa, kabla ya
    kwenda kuondolewa nyuzi siku chache zijazo. Huku akiendelea kufanya
    mazoezi kila siku, Rais Kikwete pia ameendelea kupokea salamu za
    Watanzania kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) kutoka kila pembe ya dunia
    pamoja na salamu za kumtakia nafuu mapema kutoka kwa viongozi
    mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi wa nchi za nje. Naye
    amekuwa akizijibu kwa kadri anavyoweza.
    1Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Daktari Edward Schaeffer
    muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Johns
    Hopkins huko Baltimore, Maryland nchini Marekani ambapo alifanyiwa
    upasuaji wa kuondoa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita. Hali ya

    Rais Kikwete imezidi kuimarika baada ya kutoka wodini na kuwa
    mapummzikoni akiuguza kidonda kabla ya kwenda kuondolewa nyuzi siku
    chache zijazo. Huku akiendelea kufanya mazoezi kila siku, Rais Kikwete
    pia ameendelea kupokea salamu za Watanzania kwa njia ya ujumbe mfupi
    (SMS) kutoka kila pembe ya dunia pamoja na salamu za kumtakia nafuu
    mapema kutoka kwa viongozi mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi
    wa nchi za nje. Naye amekuwa akizijibu kwa kadri anavyoweza

    0 maoni:

    Chapisha Maoni