Chelsea
na Paris Saint-Germain zimetoka 1-1 katika Mechi ya Kirafiki ya
michuano ya International Champions Cup huko Bank of America Stadium,
North Carolina lakini Chelsea wamepata ushindi baada kupigiana Penati
kwa kupata Penati 6-5. Majuzi, Chelsea walitwangwa Bao 4-2 katika Mechi yao ya kwanza na New York Red Bulls.
Bao za mechi hii zilifungwa na Zlatan Ibrahimovic, Dakika ya 25, kwa PSG na lile la Chelsea kufungwa na Victor Moses katika Dakika ya 65.
Kwenye Mikwaju ya Penati, KIpa wa Chelsea, Thibaut Courtois, aliokoa Penati mbili. Zikiwa zimebki Dakika 25, Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alimuingiza Straika wao mpya alietoka kwa Mkopo kutoka AS Monaco, Radamel Falcao.
Kipa wa Chelsea akiachia na kumfunga kipa mwenzake wa PSG
Akiokoa mkwaju wa Penati
Radamel Falcao akipigana vikumbo kuutafuta mpira dhidi ya Marquinhosvies
Kipa wa Chelsea Thibaut akiokoa jahazi langoni mwake
Thiago Motta na John Terry
Blaise Matuidi na Nemanja Matic
Wachezaji wa PSG wakimpongeza mwenzao Zlatan baada ya kufunga bao kipindi cha kwanza
0 maoni:
Chapisha Maoni