.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatano, 25 Novemba 2015

Tagged Under:

Miaka 14 toka Zlatan Ibrahimovic ahame Malmo.. haya ndio mapokezi atakayokutana nayo!!

By: Unknown On: Jumatano, Novemba 25, 2015
  • Share The Gag

  • Usiku wa leo kutakuwa na mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya kati ya PSG ya Ufaransa dhidi ya klabu ya Malmo ya Sweden.
    Zlatan Ibrahimovic atakuwa nyumbani katika mji wa Malmo, Sweden wakati atakapokuwa na timu yake…lakini mashabiki wa nyumbani wameamua kuonyesha heshima kubwa kwake kwa kumkaribisha kwa staili ya aina yake ikiwa ni miaka 14 tangu aihame timu hiyo ya nyumbani.
    mji
    Moja ya makumbusho ya jengo lililojengwa mwaka 1546 mjini Malmo ambapo kumeandaliwa tafrija ya kumpokea Zlatan.
    Jengo refu kuliko yote katika mji huo wa Malmo umepambwa kwa herufi kubwa ya Z ikiwa na maana ya jina lake Zlatan.Hii ni moja ya ishara ya kumkaribisha tena staa huyo lakini safari hii akiwa na timu ya ugenini.
    jina
    Jengo refu zaidi Sweden lililopambwa kwa herufi Z likimaanisha Zlatan
    Zlatan amewaambia  mashabiki wa Malmo wanaweza kuimba jina lake kama walivyokuwa wakifanya awali wakati akiitumikia timu hiyo.

    mahakama
    Malmo ndiyo ilikuwa timu yake ya kwanza kubwa iliyomkuza kisoka kabla ya kununuliwa na Ajax ya Uholanzi.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni