BEKI
wa Manchester United Luke Shaw anatarajiwa kufanyiwa operesheni ya pili
Ijumaa kutibu Mguu wake wa Kulia uliovunjika Mifupa yote miwili kwenye
ugoko.
Shaw
aliumizwa na Beki wa PSV Eindhoven Hector Moreno katika Dakika ya 15 ya
Mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI Jumanne Usiku huko Netherlands wakati Man
United wanafungwa 2-1 na PSV na kupelekwa Hospitali ya St Anna
Ziekenhuis iliyoko nje tu ya Jiji la Eindhoven na Usiku huo huo
kufanyiwa operesheni iliyosimamiwa na Madaktari Wawili Mabingwa wa
Mifupa na Mtaalum wa Ajali.Mkurugenzi Mtendaji wa Man United, Ed Woodward, ameshamtembelea Shaw na Wazazi wake wamesafirishwa kumwona Mtoto wao.
Hata mwenyewe Shaw ameleta matumaini kwa kuposti Mitandaoni maendeleo yake ambayo pia hata Meneja wa Man United Louis van Gaal amegusia kuwa huenda Kijana huyo wa Miaka 20 akarejea dimbani mapema zaidi Machi Mwakani.
0 maoni:
Chapisha Maoni