Arsene
Wenger, ambae Jose Mourinho aliwahi kumbatiza kuwa ni ‘Mtu Spesho wa
Kufeli’, ameweka Rekodi mpya huko Ulaya kwa kuwa Meneja wa kwanza wa
Klabu aliefungwa Mechi 50 za UEFA CHAMPIONS LIGI.
Huu
ni Msimu wa 18 kwa Wenger kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI akiwa na Arsenal
lakini hajawahi hata mara moja kubeba Kombe hilo na alifika Fainali mara
moja tu. Hata hivyo, licha ya takwimu hii ya kufungwa mara 50 kumdidimiza Wenger lakini pia inaonyesha mafanikio yake makubwa ya kuhakikisha Mwaka nenda rudi Arsenal inashiriki UEFA CHAMPIONS LIGI kitu ambacho hakikutwi na Meneja mwingine yeyote huko England kwa sasa.
0 maoni:
Chapisha Maoni