Jumatatu, 21 Septemba 2015
Tagged Under:
Mgombea urais wa Tbanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli
akiwapungia mkono wananchi wakati wa mkutano wa kampeni za urais, ubunge
na udiwani kwenye Uwanja wa Michezo mjini Chato, mkoani Geita, jimbo
alilokuwa Mbunge. Pia alitumia fursa hiyo kuwaaga wapiga kura
wake.Mkutano huo wa kampeni ulijaza watu kupita kiasi jambo ambalo
wenyeji wa wilaya hiyo pamoja na mgombea amesema haijawahi kutokea.PICHA
ZOTE NA RICHARD BMWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mbuzi huyu aliyechorwa maandishi hayo aliletwa kwenye mkutano huo na mmoja wa wafuasi wa CCM kwa lengo la kuwakebehi Ukawa.
Dk. Magufuli akijinadi kwa wananchi wa Wilaya ya Chato ili wampigie kura nyingi yeye pamoja na mbunge na diwani wa CCM.
Dk Magufuli akiwahidi wananchi kuwa akipewa ridhaa ya kuongoza nchi
atahakikisha elimu ya bure inatolewa kuanzia shule za msingi hadi
kidato cha nne
Mke wa Mgombea urais wa Tganzania kupitia CCM, Janeth Magufuli
akipongezwa na mumewe, Dk Magufuli baada ya kutoka kumuombea kura
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakitumbuiza wakati wa mkutano huo
Baadhi ya wananchi wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti
Baadhi ya wapigapicha za habari wakiwa juu ya magari kwa lengo la
kupata picha nzuri wakati msafara wa Dk Magufuli ulipokuwa ukitokea
nyumbani kwao kwenda kwenye mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Michezo
mjini Chato leo
Dk Magufuli akiingia kwenye mkutano wa kampeni mjini Chato
Kikundi cha ngoma za asili cha Mchele Mchele kikitumbuiza katika mkutano huo
Wanamuziki wa Yamoto Band wakitumbuiza wakati wa mkutano huo
Wafuasi wa CCM wakionesha dole gumba ikiwa ni ishara ya kumkubali Dk Magufuli kuwa rais
Msanii Khadija Kopa wa Kikundi cha Sanaa cha CCM cha TOT, AKITUMBUIZA KWA WIMBO WA TAARABU WAKATI WA KAMPENI HIZO
Wasanii wengine wakiendelea kuunga mkono Malkia wa Mipasho Khadija Kopa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, Abdallah Bulembo akielezea wasifu
wa Dk. Magufuli uliomfanya ateuliwe na CCM kuwa mgombea urais wa
Jamhuri ya Tanzania.
Dk Magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Josph Musukuma wakati wa kampeni hizo
Mwakilishi wa watu wenye ulemavu wana CCM na wasio wanaCCM, Amon
Mpanju akihutubia kwa kuelezea ubaya wa Ukawa na kusifia CCM ambayo
alidai inawajali walemavu nchini.
Kampeni za Dk. Magufuli kwao Chato ni zaidi ya Tsunami
By:
Unknown
On: Jumatatu, Septemba 21, 2015
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 maoni:
Chapisha Maoni