.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Ijumaa, 25 Septemba 2015

Tagged Under:

CARLO ANCELOTTI NA JURGEN KLOPP WAMNYIMA USINGIZI KOCHA BRENDAN RODGERS ANFIELD!

By: Unknown On: Ijumaa, Septemba 25, 2015
  • Share The Gag
  • MENEJA wa Liverpool Brendan Rodgers anakabiliwa na Siku 10 zenye Mechi 3 ambazo zitaamua kama ana kibarua au la huku kukiwa na uvumi Mtaliana Carlo Ancelotti au Mjerumani Jurgen Klopp wanaandaliwa kutwaa nafasi yake.
    Baada ya kushuhudia Jumatano Usiku Liverpool ikitolewa jasho na Timu ya Daraja la chini Ligi 2, Carlisle, Uwanjani Anfield na kwenda Sare 1-1 na hatimae kushinda kwa Penati 3-2 kwenye Mechi ya Raundi ya 3 ya Capital One Cup, Wachambuzi wanahisi sasa muda wa Brendan Rodgers kubwagwa umefika.
    Katika Mechi zao mbili zijazo, Liverpool watakabiliana na Aston Villa na Mahasimu wao wakubwa Everton katika Ligi Kuu England lakini katikati ya Mechi hizo, Liverpool itacheza Mechi ya Kundi lao la EUROPA LIGI dhidi ya Sion.

    Msimu huu, Liverpool walishinda Mechi zao mbili za kwanza dhidi ya Stoke na Bournemouth lakini baada ya hapo wakaenda Gemu 5 bila ya ushindi.
    Lakini Wachambuzi wamedai hata huo ushindi dhidi ya Stoke na Bournemouth ulikuwa wa Bao 1-0 tu na ulikuja kibahati huku ule waliopata dhidi ya Bournemouth ulikuja kwa Bao la Christian Benteke wakati Philippe Coutinho akiwa Ofsaidi.
    Brendan Rodgers alipewa sapoti na Wamiliki wa Liverpool, Fenway Sports Groups, kwenye Msimu uliopita ambao ulikuwa mbovu kwao lakini sasa inaaminika kuwepo huru kwa Mameneja mahiri Carlo Ancelotti, aliewahi kuziongoza AC Milan, Chelsea, Paris St-Germain na Real Madrid, na Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund, Jurgen Klopp, kumefanya awe kwenye hali tete.


    0 maoni:

    Chapisha Maoni