.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumanne, 22 Septemba 2015

Tagged Under:

DI MARIA: NIKIIFUNGA REAL MADRID, SITASHANGILIA HATA KIDOGO

By: Unknown On: Jumanne, Septemba 22, 2015
  • Share The Gag
  •  Kiungo mwenye kasi wa PSG, Angelo Di Maria amesema hatashangilia kama atafanikiwa kufunga bao wakati wakivaa Real Madrid.


    Di Maria ametua PSG akitokea Manchester United ambayo ilimnunua kutoka Real Madrid ambayo sasa wako nayo kundi moja katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

    Madrid itaanza kukutana na Madrid Oktoba 21 jijini Paris, Ufaranda kabla ya kurudia Madrid Novemba 3.
     
    “Nilipojua ninahamia PSG nilimueleza mke wangu hofu ya kwamba tunaweza kupangwa na Real Madrid. Nilianza kujiuliza watanipokeaje siku nikienda pale na timu nyingine.

    “Tumekuwa pamoja, tulishinda makombe mengi kwa pamoja na walinionyesha heshima kubwa. Mfano baada ya kujua ninaenda Manchester United, uwanja mzima walisimama kuniaga.

    “Ni watu walioonyesha upendo mkubwa kwangu, itakuwa vigumu kushangilia kama nitafunga ingawa nitacheza kwa juhudi kubwa kwa ninataka mafanikio pia nikiwa PSG, nataka kushinda makombe,” alisisitiza Di Maria.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni