.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 24 Septemba 2015

Tagged Under:

KUZIONA SIMBA vs YANGA 7000/, TIKETI KUUZWA KUANZIA IJUMAA!

By: Unknown On: Alhamisi, Septemba 24, 2015
  • Share The Gag

  • Viingilio vya mchezo wa watani wa jadi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania utakaochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam vimetangazwa leo ambapo kiingilio cha chini kitakua ni shilingi elfu saba (7,000).
    atika mchezo huo kiingilio cha juu kitakua ni shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa viti vya VIP A, Elfu Ishirini (20,000) kwa viti vya VIP B & C, huku kiingilio cha shilingi Elfu Saba (7,000) kikiwa ni kwa viti vyenye rangi ya Blu, Kijani na Orange.
    Tiketi za mchezo ho zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa saa 2 kamili asubuhi katika vituo vifuatavyo: Karume – Ofisi za TFF, Buguruni – Oilcom, Dar Live – Mbagala, Uwanja wa Taifa, Luther House – Posta, Ferry – Kivukoni, Mnazi Mmoja, Ubungo – Oilcom na Makumbusho – Standi ya mabasi ya daladala.
    TFF inawaomba wapenzi, wadau na washabiki wa mpira wa miguu nchin kununua tiketi katika magari yaliyopo kwenye vituo vya kuuzia tiketi ili kuondokana na kuuziwa tiketi zisizo sahihi.
    Mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi wa kimataifa mwenye beji ya FIFA, Israel Nkongo (Dsm) akisaidiwa na Josephat Bulali (Tanga), Ferdinand Chacha (Mwanza) mwamuzi wa akiba Soud Lila (Dsm) wakati kamisaa wa mchezo huo atakua Charles Mchau kutoka Kilimanjaro.
    Michezo mingine ya Ligi Kuu ya Vodacom siku hiyo ya Jumamosi itakua ni kati ya Coastal Union dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Maafande wa jeshi la Magereza (Tanzania Prisons) watawakaribisha maafande wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni