
Timu ya West Ham United sasa wamekuwa mafundi wa kuzibomoa Timu kubwa Nyumbani kwao Msimu huu baada ya Jana kuwatandika Vinara wa Ligi Kuu England Manchester City Bao 2-1 wakiwa kwao Etihad na kuwaonjesha kipigo chao cha kwanza kwenye Ligi Msimu huu.
Kipigo hiki pia ni cha pili mfululizo kwa City ambao Kati-Wiki walichapwa 2-1 na Juventus hapo hapo Etihad kati Mechi ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONS LIGI.

Jana huko Etihad, West Ham, chini ya Meneja wao mpya kutoka Croatia Slaven Bilic, walitangulia kwa Bao 2 zilizofungwa na Mchezaji wa Mkopo kutoka Chelsea Victor Moses katika Dakika ya 6 na Diafra Sakho katika Dakika ya 31.
Bao la City lilifungwa na Mchezaji wao mpya Kevin De Bruyne katika Dakika ya 46.
Hadi Mapumziko City 1 West Ham 2.
Kipindi cha Pili, City, waliocheza bila ya Mastaa wao Majeruhi, Vincent Kompany na David Silva, walikuja juu lakini West Ham walisimama kidete kulinda Bao zao.



0 maoni:
Chapisha Maoni