.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumanne, 10 Machi 2015

Tagged Under:

WAKUU WA MIKOA YA MBEYA NA RUKWA WAMTEMBELEA MTOTO ALBINO ALIYEKATWA KIGANJA

By: Unknown On: Jumanne, Machi 10, 2015
  • Share The Gag
  • Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya, Dk. Mpoki Ulisubisya akiwaongozwa Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Rukwa kuelekea Wodini kumjulia hali Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi.
    Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi akiwa amelala kitandani akiendelea kupatiwa matibabu.
    Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stellah Manyanya akiwa anamwangalia kwa jicho la huruma Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana na kutokomea nacho akiwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
    Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Rukwa wakimjulia hali Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi.
    Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Rukwa sambamba na viongozi wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya wakiwa wameinamisha nyuso zao huku wakisali kuwaombea watu wenye ulemavu wa ngozi ili wasipate madhara baada ya kumtembelea Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi.
    Mama mzazi wa mtoto Baraka,Prisca Shabani akiwa na jeraha kichwani baada ya kupigwa na watu waliomkata kiganja mtoto wake, akiwa anawasikiliza wakuu wa mikoa ya Mbeya na Rukwa waliomfika kuwajulia hali katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya wanakopatiwa matibabu.
    .Waandishi wa habari wakichukua maelezo kutoka kwa wahanga wa tukio la kukatwa kiganja kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino).

    0 maoni:

    Chapisha Maoni