.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatano, 23 Septemba 2015

Tagged Under:

NJOO TUSHEHEREKEE PAMOJA KWENYE MKESHA WA EID NA SKYLIGHT BAND LEO NDANI YA KIOTA CHA ESCAPE ONE MIKOCHENI

By: Unknown On: Jumatano, Septemba 23, 2015
  • Share The Gag


  • Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower( kushoto) akiendelea kutoa burudani ya nguvu huku msanii mwenzake Sony Masamba akiendelea kuzirundi ngoma ndani ya kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar. Usikose leo siku ya Jumatano kwenye mkesha wa EID maana kuna vitu vingi vipya.

    Mwimbaji wa Bendi ya Skylight, Natasha pamoja na mwenzake Kasongo Junior haya ni Majembe mapya ya bend ya Skylight yenye uwezo mkubwa wa katika uimbaji.

    Sony Masamba ambaye ni mmoja wa waimbaji wa Skylight akiendelea kutoa burudani akisindikizwa na waimbaji wenzake.

    Sam Mapenzi pamoja (kulia) akiimba pamoja na Ashura Kitenge wakiendelea kuwakonga nyoyo mashabiki wa Skylight Band waliofika siku ya Jumapili kwenye kiota cha Escape One Mikocheni na leo sio ya kukosa njoo tukeshe pamoja tukifurahi na mziki mzuri kutoka katika bendi hiyo.

    Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiimba huku mashabiki wa bendi hiyo wakiserebuka kwa furaha na leo sio ya kukosa njoo na mwenzako uje kuona vitu vipya kutka kwenye bendi hiyo.
    Mwimbaji wa Bendi ya Skylight, Natasha akiendelea kutuoa burudani kwa mashabiki wao waliofika kwenye kiwanja cha Escape One kujionea burudani ya nguvu kutoka katika bendi hiyo.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni