.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatatu, 21 Septemba 2015

Tagged Under:

LA LIGA: MESSI AKOSA PENATI, APIGA 2, BARCA WAKIINYUKA BAO 4-1 LEVANTE!

By: Unknown On: Jumatatu, Septemba 21, 2015
  • Share The Gag

  • MABINGWA Watetezi wa La Liga, FC Barcelona, wameendelea kujikita kileleni mwa Ligi hiyo ya Spain baada ya Jana Usiku wakiwa kwao Nou Camp kuichapa Levante Bao 4-1.
    Licha ya kukosa Penati katika Dakika ya 75, Lionel Messi alifunga Bao 2, moja likiwa pia Penati ya Dakika ya 61 na jingine kwenye Dakika ya 90. Bao nyingine za Barca zilifungwa na Marc Bartra Dakika ya 50 na Neymar Dakika ya 56. Bao pekee la Levante lilifungwa na Victor Casadesus katika Dakika ya 66.
    Ushindi huu umewafikisha Barcelona Pointi 12 baada ya kushinda Mechi zao zote 4 na kuongoza La Liga wakifuatiwa na Real Madrid wenye Pointi 10 wakiwa wamefungana kwa Pointi na Villareal na Celta Vigo.
    La Liga itaendelea tena kati ya Wiki kwa Mechi za Jumanne, Jumatano na Alhamisi.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni