.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatatu, 21 Septemba 2015

Tagged Under:

MPANGO WA NGOMA AIUE SIMBA UMEANZA KUSUKWA.....

By: Unknown On: Jumatatu, Septemba 21, 2015
  • Share The Gag


  • Huku presha ikiwa ndiyo inazidi kupanda kuelekea mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga ambao utapigwa wikiendi hii, straika Mzimbabwe wa Yanga, Donald Ngoma, anaandaliwa mpango maalumu na wachezaji wa timu hiyo kwa ajili ya kuzitikisa nyavu za Simba.


    Ngoma ambaye mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao matatu, kwa mara ya kwanza atakuwa anashiriki mchezo huo wa Simba na Yanga.

    Mshambuliaji mwenye kasi wa timu hiyo, Simon Msuva, alisema kuwa kwa sasa wapo katika mazoezi maalumu ya kuhakikisha wanamng’arisha Ngoma katika mchezo huo kwa kumtengenezea nafasi nyingi za kufunga.

    “Sisi kama washambuliaji tupo katika mpango maalumu wa kuhakikisha tunamfanya Ngoma aweze kuifunga Simba pale ambapo tutakutana katika mchezo wetu wa ligi kuu wikiendi hii.

    “Mpango huo tumeuandaa na Tambwe ambapo itakuwa ni kuhakikisha tunapiga pasi za mwisho kwa Ngoma, kwani mabeki wa timu pinzani watakuwa wanatutolea macho sisi kutokana na kutujua kwa ukaribu.


    “Lakini pia kama mchezo huo ikitokea penalti yoyote ile basi yeye (Ngoma) ndiye atakuwa mpigaji na sisi kukaa pembeni na hata kufunga kwetu itakuwa nadra, labda itokee nafasi ambayo itakuwa inaturuhusu kufanya hivyo,” alisema Msuva.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni