MASHABIKI
wa Manchester City sasa wamekuwa mbogo na kuanza kumshambulia Meneja
wao Manuel Pellegrini baada ya Jumamosi kunyukwa 4-1 na Tottenham kwenye
Mechi ya Ligi Kuu England. Wiki mbili zilizopita Man City walikuwa kileleni mwa Ligi Kuu England baada ya kushinda Mechi zao zote 6 za Ligi Kuu England lakini sasa wamechapwa Mechi mbili mfululizo na kupokonywa uongozi wa Ligi na Mahasimu wao wakubwa Man United.
Kwa Mashabiki wengi wa Man City kuporomoka kwao ni kosa la Manuel Pellegrini na uamuzi wake wa kumpiga Benchi Kipa wao Joe Hart na kumchezesha walipochapwa 4 na Spurs haukupokelewa vyema.
Baadhi
ya Mashabiki hao wamediriki hata kudai Pellegrini ni Meneja wa kawaida
tu na hastahili kuongoza Timu yao yenye Wachezaji wenye hadhi ya
Kisupastaa.
Harry Kane
0 maoni:
Chapisha Maoni