James Milner wa Man City ajiunga na Liverpool.Liverpool wameafikiana Dili ya kumsaini Kiungo wa England James Milner ambae anachezea Manchester City kwa Uhamisho wa bure.
Milner, mwenye Miaka 29, ameshakubaliana malupulupu yake binafsi na Liverpool na atajiunga rasmi nao kama Mchezaji Huru wakati Mkataba wake na City utakapomalizika hapo Julai Mosi kama akifuzu upimwaji Afya yake.
Akiwa na City kwa Miaka Mitano, Milner alifanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 2, FA CUP na Kombe la Ligi, Capital One Cup.
Milner pia ameichezea England mara 53. Msimu uliopita, Milner alianza Mechi 24 na kufunga Bao 8 na kuifungia City Bao 8.
Mchezaji huyu alijiunga na City iliyokuwa chini ya Roberto Mancini Mwaka 2010 kwa Dau la Pauni Milioni 26 akitokea Aston Villa na kuichezea Klabu hiyo jumla ya Mechi 125 na kufunga Bao 18.
Klabu nyingine alizowahi kuzichezea ni Newcastle United na Klabu ya Mji wa Nyumbani kwao Leeds United ambayo alianza kucheza Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza Mwaka 2002 akiwa na Miaka 16 tu.
Ilkay Gundogan
Memphis Depay wa PSV - Ni wa Manchester United mpaka sasa akitokea PSV Eindhoven
Morgan
Schneiderlin kujiunga na Klabu ya Man United baada ya kushinda mbio
hizo huku Klabu ya Arsenal nayo ikiwa kwenye mchakato huo huo wa
kumwania mchezaji huyo.
Christian Atsu wa Chelsea atua kwa Mkopo Bournemouth
Philipp - Bayer Leverkusen kwenda Stoke
Xavi - Al -Sadd
Kipa Artul Borus - Southampton kwenda Bournemouth
Graham Dorrans - West Brom kwenda Norwich
Joshua King - Blackburn kwenda Bournemouth
Winger wa Benfica Nicolas Gaitan nae inasemekana kujiunga na Man United
Boyata wa Man City kwenda Celtic
Luiz Gustavo anukia Old Trafford
0 maoni:
Chapisha Maoni