Paul Scholes, Andy Cole wakifurahia pamoja na Louis Saha
Wimbo kabla ya Mechi
Manahodha wa Timu Paul Scholes na Paul Breitner wakiingia Uwanjani
Kikosi
cha Man United, akiwemo Paul Scholes, Edwin van der Saar, Dwight Yorke
na wengine kwenye mchezo uliowakutanisha Magwiji hao wa soka na kucheza
mchezo dhidi ya wajerumani Timu ya Bayern Munich(Magwiji) kwenye Uwanja
wa Old Trafford.
Andy Cole akichuana na Mchezaji gwiji wa Bayern Munich Daniel Van Buyten
Park Ji-Sung akituliza mpira kiuzuri
Luis Saha ndie aliyeifungia Man United bao la kwanza.Kwenye Mechi ya Hisani iliyochezwa hii Leo huko Old Trafford, Malejendari wa Manchester United wamewatwanga wenzao wa Bayern Munich Bao 4-2 mbele ya Mashabiki 50,128.
Mwaka Jana kwenye Mechi kama hii iliyochezwa huko Allianz Arena Jijini Munich, Timu hizi zilitoka Sare ya 3-3.
Katika Mechi ya Leo, Mabao ya Man United yalifungwa na Luis Saha, Dakika ya 9, Dwight Yorke, 39, Andy Cole, 45, na Jesper Blomqvist, 83, wakati yale ya Bayern yalifungwa na Zickler , Dakika ya16, na Tarnat, 42.
Luis saha akipongezwa na Andy cole
Mchezaji wa zamani wa Bayern Alexander Zickler akichuana na Jaap Stam
Paul Scholes akiendesha
Mchezaji wa zamani wa Bayern Alexander Zickler ndie aliyeipatia bao la kwanza Bayern Munich
Dwight Yorke aliipa bao la pili Man United na kufanya 2-1
Dwight Yorke akishangilia bao lake
Wakipongezana
Phille Neville akiachia shuti
Michael Tarnat aliifungia bao la pili Bayern Munich
Wakipongezana na Paulo Sergio
Michael Tarnat akifurahia bao lake
Ji Sung park akibanwa
Andy Cole lifunga la tatu
Scholes akifanya yake
Quinton Fortune akishangilia
Jesper dhidi ya Robert Kovac
0 maoni:
Chapisha Maoni