.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 25 Juni 2015

Tagged Under:

COPA AMERICA: WENYEJI CHILE NUSU FAINALI, KUWAPIGA URUGUAY BAO 1-0.

By: Unknown On: Alhamisi, Juni 25, 2015
  • Share The Gag

  • Wakicheza kwao Estadio Nacional de Chile, Santiago, Chile wameifunga Mtu 9 Uruguay Bao 1-0 na kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Marekani ya Kusini, COPA AMERICA.
    Bao hilo la Chile lilifungwa na Mauricio Isla katika Dakika ya 81 wakati Uruguay, Mabingwa Watetezi, wakicheza Mtu 10 baada ya Edinson Cavani kutolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 63 kufuatia Kadi ya Njano ya PIli.Cavani alipewa Kadi ya Njano ya kwanza katika Dakika ya 29.
    Katika Dakika ya 88 Uruguayl ilibaki Mtu 9 baada Jorge Fucile kupewa Kadi Nyekundu baada kujizolea Kadi za Njano mbili.
    Kwenye Nusu Fainali, Chile watacheza na Mshindi kati ya Bolivia na Peru wanaocheza Usiku huu.
    RATIBA
    ROBO FAINALI
    Jumatano Juni 24

    Chile 1 vs Uruguay 0
    Alhamisi Juni 25
    Bolivia vs Peru (Saa 8:30Usiku)
    Ijumaa Juni 26
    Argentina vs Colombia (Saa 8:30Usiku)
    Jumamosi Juni 27
    Brazil vs Paraguay (Saa 6:30 Usiku)
    NUSU FAINALI
    Jumatatu Juni 29

    Chile vs Bolivia/Peru (Saa 8:30 Usiku)
    Jumanne Juni 30
    Argentina/Colombia vs Brazil/Paraguay (Saa 8:30 Usiku)

    0 maoni:

    Chapisha Maoni