.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Ijumaa, 19 Juni 2015

Tagged Under:

Baada ya kutua kutoka Marekani Ali Kiba atangazwa kuwa Balozi!

By: Unknown On: Ijumaa, Juni 19, 2015
  • Share The Gag
  • Good news ninayotaka kukusogezea ni kwamba Msanii wa Bongo Fleva Ali Kiba, Jacqueline Ntubaliwe , Vanessa Mdee wameamua kuungana na shiriki la kimataifa liitwalo WildAid ili  kupiga vita ya ujangili na biashara ya pembe za ndovu.
    Uzinduzi wa kampeni hiyo ulifanyika katika hoteli ya Sea Cliff na kuhudhuliwa na waziri wa Maliasili na Utali, Lazaro Nyalandu na wakiwemo mabarozi wa china na marekani.
    Akizungumza na waandishi wa habari Ali Kiba alisema ‘Nashukuru kwanza nilipata nafasi ya kuishi na tembo porini kwa muda wa siku wa tatu kwa hiyo kiukweli lazima uogope maana mimi ni muoga nambari moja,  ila nilichokuwa nafikiria ni tofauti na vile nilivyodhani ila tembo ni wanyama wazuri
    .
    .
    Vile vile nilipata nafasi ya kwendaNairobi kuwatembelea watoto wa tembo yatima mama zao wameuliwa na watu wasio na imani ukifikiri kibinadamu wanyama ni viumbe kama sisi, kuna wale ambao tumeruhusiwa kula lakini sio kwa wale ambao ni fahari kwetu sisi ni vivutio vinaipa nchi yetu thamani, wageni wanakuja kuona hao hao wanyama wetu lakini watu wanawaua kwasababu unavyowatoa ndovu zao ni sawa sawa unawatesa wanaumia kiukweli mimi napiga vita hivi vya ujangili lakini kutokana na imani na kutaka Tembo hao wanapata watetezi ambao ni sisi, mimi na yoyote kwani wale ni kama raia na pia wana haki ya kuishi ndio maana tukiwa na mapenzi nao tunaenda kuwaona, kwa hiyo mimi hili suala nimelipokea kwa mikono miwili na nimefuraha kuwa balozi wa WildAid, nimetembelea sehemu nyingi kama Tarangire na bado nitaendelea kutembelea na wengine mnakaribishwa kutembelea hifadhi za wanyama.
    Kwa hiyo na imani mimi na wasanii wengine ambao tunaweza tukatimia nguvu hii ya pamoja, Jacqueline Mengi na Vanessa Mdee kwakweli tuko mbele juu ya suala hili, ningependa sana watanzania tushirikiane katika jambo hilo unapoona tukio hilo limetokea basi toa taarifa mapema kwani ujangili unatuumiza sisi sote…..’alisema.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni