.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumamosi, 27 Juni 2015

Tagged Under:

Hii ndio hofu kubwa kuliko zote ya P-Square katika maisha yao!

By: Unknown On: Jumamosi, Juni 27, 2015
  • Share The Gag



  • Peter Okoye na Paul Okoye ni wasanii mapacha kutoka Nigeria ambao pamoja wanauda kundi maarufu la P-Square, kundi ambalo lina umaarufu mkubwa sana Africa kwa kutengeza hit songs nyingi sana, na mara nyingi wasanii hawa hutengeneza ngoma zao kupitia  studio yao ya Square Records.
    December mwaka 2011 kundi hili liliingia mkataba na lebo ya Akon Konvict Muzik na kupitia lebo hio waliweza kuachia ngoma kali Beautiful Onyinye walionshirikisha Rick Ross na Chop Ma Money zilizohit na kupata airtime kubwa kwenye redio mbali mbali Africa na mwaka 2012 kundi hili liliingia mkataba na Universal Music ya South Africa wa kusambaza nyimbo zao sehemu zote Africa.
    So mafanikio ya P-Square yanasukumwa na nini haswa? Kama kundi wanahofia nini haswa katika levo ya mafanikio walionayo? kwenye interview moja waliofanya Nigeria P-Square walisema haya;
    PS >>> “Siri ya mafanikio yetu ni kazi.Tunafanya sana kazi, sana! Juhudi zote hizi tunazowekeza katika kazi yote ni hofu ya umasikini, tumesha onja maisha ya umasikini mkubwa na tunauogopa sana umasikini na ndio maana utasikia tunawekeza hapa na kule yote ni kujikinga na umasikini ambao ukifanya mzaa sio kitu kigumu kupata, pia tumeshuhudia wasanii waliopata umaarufu na utajiri kabla yetu lakini leo hawana chochote cha kuonyesha kwa juhudi zao, kitu hiki kinatuogopesha sana. Pia sisi tulishawahi kuishi maisha ya kubanana baba,mama na watoto nane kwenye nyumba ya kupanga yenye vyumba viwili, chakula, ada, mavazi vilikua ni tatizo sana kwetu na ndio kipindi hicho baba yetu alitusihi sana tuje kuwa mabossi wa maisha yetu wenyewe tusiopenda kufanya kazi chini ya mtu na ndio maana unawaona P-Square wanafanya biashara zao wenyewe leo”.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni