.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumanne, 16 Juni 2015

Tagged Under:

TAIFA STARS YAWASILI VIONGOZI WACHEZAJI NA BENCHI LA UFUNDI WATOKA MMOJA MMOJA KUKWEPA WAANDISHI

By: Unknown On: Jumanne, Juni 16, 2015
  • Share The Gag






  • TIMU ya soka ya taifa, Taifa Stars leo imerejea nchini kutoka Misri ilipokwenda kucheza mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwishoni mwa wiki iliyopita na kufungwa mabao 3-0.
    Kwa muda mrefu Stars haijapata matokeo mazuri kwenye mechi za kimataifa hali iliyofanya wachezaji wake kutoka uwanja wa ndege kwa mafungu huku wengine wakikwepa kuzungumza na vyombo vya habari.
    Timu hiyo iliwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere saa 7:30 mchana na wachezaji wake kuanza kutoka mmoja mmoja wakiongozwa na Juma Abdul, kisha akafuata Salum Telela, Amri Kiemba, Aggrey Moris na Jonas Mkude.
    Tofauti na siku za nyuma, mashabiki hukusanyika kuipokea timu hiyo pamoja na viongozi mbalimbali, leo hali ilikuwa tofauti hakukuwa na kiongozi yeyote uwanjani hapo si kutoka Shirikisho la soka Tanzania (TFF) wala kwa wadau wa soka.
    Kila mchezaji alipotoka, madereva taxi wa uwanja wa ndege  walisema: “Eeh watalii mmerudi, watalii mmerudi,”.
    Akizungumza uwanjani hapo, mchezaji wa kimataifa anayecheza TP Mazembe ya Congo DR, Mbwana Samatta alisema hakuna ubishi kwamba walicheza na timu bora na kilichobaki ni kujipanga upya.
    “Ni kweli mechi ilikuwa ngumu sana kama mlivyoona… tulifungwa sababu muda mwingi tulikuwa tunazuia, sasa unategemea nini? si unachoka,” alisema Samatta.
    Naye nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub alisema anajua watanzania wanaumizwa na matokeo hayo lakini wasikate tamaa, wanaahidi watafanya vizuri kwenye mechi dhidi ya Uganda Jumamosi ( Kuwania kufuzu fainali za mataifa kwa wachezaji wa ndani, CHAN)  ili kurudisha imani.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni