.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 11 Juni 2015

Tagged Under:

LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA: VODACOM KUTOA ZAWADI KWA MCHEZAJI BORA, PAMOJA NA WASHINDI WENNGINE WA VPL KESHO

By: Unknown On: Alhamisi, Juni 11, 2015
  • Share The Gag

  • Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa kushirikiana na wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, kesho siku ya alhamis tarehe 11/06/2015 wanatarajia kutoa zawadi kwa washindi wa Vodacom Premier League msimu wa 2014/2015.
    Hafla ya utoaji wa zawadi hizo itafanyika katika ukumbi wa JB Belmonte (Kilimanjaro) uliopo katika jengo la Golden Jubilee Tower (PSPF), mtaa wa Ohio eneo la Posta Mpya jijini Dar es salaam kuanzia saa 12 jioni.
    Mgeni rasmi katika halfa hiyo ya utoaji zawadi kwa wachezaji, makocha, na timu washindi atakua ni Juma Nkamia, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
    Vodacom watatoa zawadi kwa Bingwa wa Ligi Kuu msimu 2014/2015, mshindi wa pili, mshindi wa tatu na mshindi wa nne, baadhi ya vipengele vitakavyotolewa zawadi pia na wadhamini hao wa Ligi Kuu ni :

    1. Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
    Mohamed Hussein (Simba SC)
    Mrisho Ngasa (Young Africans)
    Saimon Msuva (Young Africans)

    2. Mlinda mlango bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
    Mohamed Yusuph (Tanzania Prisons)
    Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
    Shaban Hassan (Coastal union)

    3. Kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
    Goran Kopunovic (Simba SC)
    Hans Van Der Pluijm (Young Africans)
    Mbwana Makata - (Tanzania Prisons)

    4. Mwamuzi bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
    Israel Mjuni Nkongo
    Jonesia Rukyaa
    Samwel Mpenzu

    5. Timu yenye nidhamu Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
    Mgambo JKT
    Mtibwa Sugar
    Simba SC

    JOHN MAHUNDI MCHEZAJI BORA MWEZI MEI
    Wakati huo huo mchezaji John Mahundi wa timu ya Coastal Union amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Mei, 2015 na jopo la makocha kufuatia kuwazidi wachezaji wengine 14 aliokuwa anananiwa nao nafasi hiyo.
    Kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi mei, Mahundi atazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni