.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 11 Juni 2015

Tagged Under:

MARTA VIEIRA DA SILVA AWEKA HISTORIA KOMBE LA DUNIA

By: Unknown On: Alhamisi, Juni 11, 2015
  • Share The Gag

  • Mshambuliaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Brazil Marta Vieira da Silva almaarufu Marta ameweka historia ya kuwa mfungaji bora wa michuano ya kombe la dunia la wanawake baada ya kufikisha mabao 15.
    Marta amefikisha idadi hiyo ya mabao baada ya kufunga bao moja kwa mkwaju wa penati kwenye mchezo wa timu yake dhidi ya korea kusini ambapo Brazili waliibuka kidedea kwa mabao 2-0.
    Ushindi huo umeifanya Brazil kuwa vinara wa kundi E, Baada ya Hispania na Costa Rica kwenda sare ya kufungana 1-1.

    Mshambuliaji huyu ameichezea timu ya taifa jumla ya michezo 137 akiwa kafunga mabao 93. Kwa sasa Marta ni mchezaji wa klabu ya Rosengard FC ya Sweden.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni