Tagged Under:
KOCHA KERR WA SIMBA AWASILI PAMOJA NA KOCHA WA MAKIPA MKENYA IDD SALIM
By:
Unknown
On: Ijumaa, Juni 26, 2015
KOCHA mpya wa Simba, Muingereza Dylan Kerr amesema ataendeleza wachezaji chipukizi ili kuwa na timu bora kwa sasa na baadae.
Kerr
aliyasema hayo baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere na kulakiwa na wajumbe wa Kamati ya Simba, Collin
Frisch na Said Tully.
“Nimefurahi kuja Tanzania na nawaahidi
viongozi na mashabiki kuwa nitahakikisha naendeleza wachezaji chipukizi
hili Simba iweze kutamba sasa na baadae”, alisema Kerr.
Kocha huyo
ambaye amerithi mikoba ya Mserbia Goran Kopunovic amesaini mkataba wa
mwaka mmoja kuifundisha Simba ambapo atakuwa anasaidiwa na kiungo wa
zamani wa timu hiyo Suleman Matola.
Wakati Kerr akiwasili pia alikutana na kocha mpya wa
makipa Idd Salim toka Kenya ambaye naye aliwasili tayari kwa kazi yake
mpya kwenye klabu ya Simba.
Simba waliamua kuachana na Kopunovic na
kusaka kocha huyo mpya baada ya Mserbia huyo kuhitaji Simba imlipe kiasi
cha Dola za Marekani 50,000 (sh. Milioni 100) kama ada ya usajili na
mshahara wake ambapo kila mwezi atakuwa analipwa dola za Marekani 14,000
9sh. Milioni 28).
Baada ya kushindwana kwenye malipo ndipo uongozi uliamua
kumsaka kocha mpya na kumpata Kerr ambaye inasemekana atalipwa mshahara
wa dola za marekani 9,000 sawa na milioni 18 kwa mwezi.
Dylan Kerr mwenye umri wa miaka 47, aliwahi kuwa mchezaji, alicheza
beki wa kulia kwenye klabu za Leeds United, Reading, Blackpool na
nyingine nyingi za Uingereza huku akihudumu kama kocha msaidizi kwenye
timu mbalimbali katika nchi za Vietnam ambako ametoka kwenye timu ya Hai
Phong F.C. ambako alimaliza mkataba 2014.
0 maoni:
Chapisha Maoni