.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 11 Juni 2015

Tagged Under:

KOCHA WA BARCA LUIS ENRIQUE ASAINI MKATABA WA KUENDELEA KUIFUNDISHA TIMU HIYO HADI 2016/2017

By: Unknown On: Alhamisi, Juni 11, 2015
  • Share The Gag

  • Hatima ya Kocha Luis Enrique kubakia FC Barcelona sasa imekwisha baada ya kusaini nyongeza kwenye Mkataba wake.
    Katika Msimu wake wa kwanza tu na Barca, Enrique alimudu kutwaa Trebo baada kubeba Ubingwa wa Spain La Liga, Copa del Rey na juzi kuzoa Kombe la Ubingwa Ulaya, UEFA CHAMPIONS LIGI.
    Lakini licha ya mafanikio hayo ilizigaa imani kubwa ataondolewa.
    Lakini kwa kusaini nyongeza ya Mkataba itakayomweka Barca hadi mwishoni mwa Msimu wa 2016/17, utata huo sasa umekwisha.
    Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu, ndie alietangaza kuongezewa Mkataba Enrique.

    Enrique, ambae aliwahi kuzichezea Barca na Real Madrid, aliteuliwa Mwaka jana kumbadili Tata Martino ambae sasa ni Kocha wa Argentina.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni