Barcelona Mabingwa Klabu Bingwa Ulaya
Raha ya ushindi kwa Barcelona wakishangilia baada ya kunyakuwa Trebo yao kwa kuifunga Juventus bao 3-1 usiku huu huko Berlin, Bao la kwanza lilifungwa na Rakitic, Surez na Neymar

Neymar na mwenzake wakiwa vifua wazi mbele ya waandishi wa Kamera baada ya mpira kumalizika

Luis Suarez
Bao
la tatu na Ushindi lilifungwa na Neymar baada ya kuwachomoka mabeki na
kufunga bao hilo na mtanange kumalizika kwa bao 3-1 dhidi ya Juventus.
Ushindi Huu unawafanya Barca kutwaa Trebo kwa kutwaa makombe matatu kwa
msimu mmoja.
3-1
Neymar akishangilia bao lake la tatu kwenye dakika ya majeruhi 90
Meneja wa Barca hakutosha wala kupimika!!!
Raha ya Ushindi huko Berlin, Germany, kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI, FC Barcelona ya Spain waliichapa Juventus ya Italy Bao 3-1 na kutwaa Ubingwa wa Ulaya hii ikiwa ni mara yao ya 5.
Ubingwa huu wa Ulaya, katika Fainali ya 60 ya Klabu Bingwa ya Ulaya, ni wa 3 kwa Barca katika Miaka 6 iliyopita na umewapa Trebo Msimu huu, ukiwa ni Msimu wa Kwanza kwa Kocha wao Luis Enrique, baada ya pia kutwaa Ubingwa wa La Liga na Copa del Rey.
Neymar akifanya yake!
2-1 mtaipenda!!!
Kupongezana muhimu
Suarez kashamaliza!
Luis Suárez akishangilia bao lake la dakika ya 68 kipindi cha pili.
Luis Suárez dakika ya 68 aliwafungia bao la pili Barcelona na kufanya 2-1 dhidi ya Juventus.
Paul Pogba chupuchupu aumalize!
Pogba akililia penati!
La mkono lilikataliwa!!!
Kipindi
cha pili dakika ya 55 Morata aliwasawazishia bao Juventus kwa kufanya
1-1 baada ya kipa wa Barca kuutema mpira na Morata kuumalizia.
Baadhi ya wachezaji wa Barca wakipongezana baada ya kupata bao la kuongoza
Ivan Rakitic akipongezwa na Lionel Messi
Kipa wa Barca Marc -Andre shangwe!
Ivan Rakitic alivyowapachikia bao la kuongoza Barca mapema kipindi cha kwanza.
1-0 Ivan Rakitic anawapatia bao la kwanza Barca dakika ya mapema ya 4, akipewa pasi safi na Andrés Iniesta Luján
Kipa Buffon akidaka vyema mpira langoni mwake
Pirlo na Neymar wakichuana katika kipindi cha kwanza
Vidal kulia) akipagawa kwa kushika vichwa baada ya nyumba yao kuungua 1-0
Evra na Lionel Messi wakichuana
Vidal akioneshwa kadi ya Njano na Mwamuzi Cuneyt Cakir
Claudio na Suarez wakigombea kuutwa mbora kipindi cha kwanza
Vidal akimweka Chini Iniesta
Neymar akijaribu!
Kikosi cha Barcelona 
0 maoni:
Chapisha Maoni