.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumamosi, 14 Novemba 2015

Tagged Under:

MSHINDI WA SHINDANO LA TRACE MUSIC AFRIKA MTANZANIA MAYUNGA KUKUTANA NA AKON

By: Unknown On: Jumamosi, Novemba 14, 2015
  • Share The Gag


  • Mshindi wa shindano la Trace Music Stars Africa, Mtanzania Nalimi Mayunga anaziandika headlines za leo kwenye kurasa za Bongo Fleva. Baada ya kushinda shindano hilo kubwa la kusaka vipaji, Mayunga aliondoka na mkataba wa kurekodi na Universal Studio wenye thamani ya dola 500,000 ambayo kwa pesa ya sasa inagonga mpaka Tzs bilion 1!
    MAYUNGA2
    Good news kwako mtu wangu, mtu wetu Mayunga anatarajiwa kuondoka Tz siku ya Jumatatu tarehe 16 November 2015 kwenda Marekani kwa ajili ya mafunzo ya muziki pamoja na kurekodi single yake na Akon ambaye kwenye shindano la Trace Music Stars Africa alikuwa miongoni wa majaji.
    MAYUNGA3
    Akiongea na CloudsFM radio leo kupitia kipindi cha XXL, Mayunga aligusia pia kuhusu safari yake ya Marekani
    >>> “Marekani naenda Jumatatu na ninachoenda kukifanya kule ni kile kinachoongelewa kwenye media, kuwa naenda kwa ajili ya mafunzo, kufanya wimbo, na vilevile kushoot video ya wimbo nitakaoenda kuurekodi… japo kusema kweli sijajua wimbo huo utakuaje kwa sababu mpaka sasa bado sijaupata na wala sijausikia. Dili ni kwamba Akon anakuandikia wimbo mwenyewe, sema sijaupata ili niweze kujipanga, so nahisi kama anataka kunipima aone uwezo wangu…” Mayunga.
    MAYUNGA

    0 maoni:

    Chapisha Maoni