MENEJA
wa Chelsea Jose Mourinho atabakia kwenye kibarua chake kwa sasa licha
ya Jana kutandikwa 3-1 Uwanjani kwao Stamford Bridge na Liverpool kwenye
Mechi ya Ligi Kuu England ikiwa ni ni kipigo chao cha 6 katika Mechi 11
za Ligi hiyo Msimu huu. Chelsea, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, wapo Nafasi ya 15 kwenye Msimamo wa Ligi wakiwa Pointi 14 nyuma ya Vinara Man City.
Akihojiwa mara baada ya kipigo cha Jana kama anadhani hiyo ndio Mechi yake ya mwisho kama Meneja, Mourinho alijibu: “Hapana. Sifikirii hilo!”
Mourinho,
ambae hajawahi kufungwa zaidi ya Mechi 6 za Ligi katika Msimu mmoja
akiwa kama Meneja wa Chelsea, aliongeza: “Mapambano yanaendelea lakini
wakati mwingine mapambano haya ni magumu kushinda. Unaingia kwenye
mapigano na silaha nyingine!”
Jose Mourinho na wasaidizi wake na viongozi wengin wakiteta jambo
Mourinho wakijiuliza jambo
Maswali yaliyobaki bila Majibu!!!

#3-1 walinyukwa na Liverpool wakiwa nyumbani Stamford Bridge


Jose Mourinho

0 maoni:
Chapisha Maoni