Kwa mujibu wa Takwimu za CIES Football Observatory Digital Atlas, Asilimia 41 ya Wachezaji waliocheza Ligi Kuu England Msimu huu wamechezea pia Timu zao za Taifa Msimu huu huu.
Man United wapo juu kwa kutoa Wachezaji Asilimia 72 ya wale walioteuliwa na Meneja wao Louis van Gaal kucheza Mechi za Ligi Kuu England Msimu huu ambao pia waliteuliwa kucheza Timu zao za Taifa.
Ijumaa
iliyopita, Wachezaji wa Man United waliovaa Jezi za Nchi zao ni Michael
Carrick, Phil Jones, Chris Smalling, Wayne Rooney na Juan Mata ambao
walicheza wakati Spain inaichapa England 2-0, wakati Anthony Martial na
Morgan Schneiderlin walikuwa kwenye France iliyoichapa Germany ambayo
ilikuwa nayo Bastian Schweinsteiger huku Daley Blind akiichezea
Netherlands na Matteo Darmian akiichezea Nchi yake Italy.
0 maoni:
Chapisha Maoni