MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger ametamka kuwa Kiungo wao Francis Coquelin
atakuwa nje kwa kipindi kisichopungua Miezi Miwili baada ya kuumia Goti
Timu yao ilipochapwa 2-1 huko The Hawthorns na West Bromwich Albion.Pia kuumia kwa Coquelin na pigo kubwa kuelekea Mwezi Desemba ambao una Mechi mfululizo hadi Mwaka mpya.
Msimu huu, Coquelin, mwenye Miaka 24, ameikamata Namba katika Kikosi cha Kwanza cha Arsenal.
Alipoulizwa
ikiwa Kiungo huyo wa Kimataifa wa France ameumia sana, Wenger alijibu:
“Siku zote nakuwa mwangalifu lakini nadhani yupo nje si chini ya Miezi
Miwili na tunasubiri uchunguzi zaidi.”
0 maoni:
Chapisha Maoni