.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatano, 4 Novemba 2015

Tagged Under:

Alan Wanga kaeleza experience ya maisha ya Sudan, ukinywa pombe hii ndio adhabu utakayopewa

By: Unknown On: Jumatano, Novemba 04, 2015
  • Share The Gag

  • Mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya anayekipiga katika klabu ya Azam FC ya Tanzania Alan Wanga November 4 amefunguka katika Amplifaya ya Clouds FM kuhusu maisha ya Sudan, nchi ambayo utamaduni wake ni tofauti na nchi nyingi za Afrika Mashariki kama Kenya, Tanzania na Uganda.
    Awali tuliwahi kusikia stori kuhusu nchi ya Sudan ambayo sheria zake ni ngumu na utamaduni wake tofauti na utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki, Alan Wanga amejiunga msimu huu na Azam FC akitokea Al-Merreikh ambayo alidumu nayo katika kipindi cha mwaka mmoja, awali tuliwahi kusikia kuwa Sudan ukinywa pombe ni kosa kisheria? Wanga ana majibu haya.
    Allan-Wanga
    “Ni kweli kuna sheria ngumu kule kama wewe ni mchezaji ambaye hauna malengo na hujui kazi yako itakuwa vigumu sana kuishi, kule hakuna klabu za usiku wala Bar kwa wale wachezaji ambao ndio wanaanza soka Sudan ni mahali pagumu kuishi, Sudan ukipatikana na pombe au umelewa nadhani sheria yao ni kupigwa viboko 40 na kama wewe ni raia wa kigeni unaweza rudishwa nchini kwenu” >>> Alan Wanga

    0 maoni:

    Chapisha Maoni