.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumanne, 10 Novemba 2015

Tagged Under:

Henry Joseph mshahara wake wa kwanza Simba? kumbe wachezaji wa Simba wote walikuwa wanalipwa sawa?

By: Unknown On: Jumanne, Novemba 10, 2015
  • Share The Gag

  • Mchezo wa mpira wa miguu ni miongoni mwa kazi zinazotajwa kulipa mishahara mikubwa zaidi duniani, siku hizi imekuwa kawaida kusikia mchezaji huyu na yule kuwa na mshahara wenye tofauti kubwa. Kwa sasa Ligi Kuu soka Tanzania bara inatajwa kuwa ni moja kati ya Ligi zinazoongoza kwa kulipa mishahara mikubwa tofauti na baadhi ya Ligi za nchi jirani.
    henry1
    November 9 nakusogezea karibu yako sehemu ya exclusive interview ya Henry Joseph ambapo amezungumza kuhusiana na mishahara na jinsi alivyoingia Simba. Henry aliingia Simba mwaka 2006 baada ya kumaliza kidato cha nne ilikuwaje? mkataba wake je? mshahara wake?
    “Ilitokea tu kama bahati nikaitwa na mwenyekiti wa Simba alikuwa Wambura wakati ule na kocha Julio nikacheza mechi ya majaribio, baadae nikapigiwa simu, Nikapewa mkataba wa miaka miwili nikasaini hata bila kuusoma Simba tena, mshahara wakati huo bwana wachezaji wote tulikuwa tunalipwa sawa laki moja na ishirini tofauti na siku hizi” >>> Henry Joseph
    ????????????????????????????????????
    Kama utakuwa unakumbuka vizuri Henry Joseph ni kiungo wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars lakini amewahi kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Kongsvinger ya Norway ila kwa sasa yupo katika klabu ya Mtibwa Sugar ya Manungu  Turiani.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni