Bao za Kipindi cha Pili za Jesse Lingard na Juan Mata Leo zimewapa Manchester United ushindi wa Bao 2-0 walipocheza na West Bromwich Albion kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Uwanjani Old Trafford.
Mapema
Kipindi cha Pili, Lingard, mwenye Miaka 22, aliifungia Man United Bao
la Kwanza kwa shuti la kupinda na Juan Mata kuongeza Bao la Pili katika
Dakika za Majeruhi kwa Penati baada ya Anthony Martial kuchezewa Faulo
na Gareth McAuley ambae alitolewa kwa Kadi Nyekundu.
Ushindi
huu umewabakisha Man United Nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England ikiwa
ni ushindi wao wa kwanza baada ya Mechi 3 za Ligi na Mechi yao
inayofuata ni ugenini na Watford hapo Novemba 21.
Bastian Chini
Cameron nae leo kacheza na Timu ya wakubwa
Lingard akipongezwa
Jesse akiponngezwa kwa bao safi
Jesse akishangilia
De Gea nae alifurahia bao
Shangwe!
Martial akichuana na Evans
Wakiunga Ukuta
Wanajuana: Rooney na Fletcher

0 maoni:
Chapisha Maoni